15Yeyote atakaye mpiga baba au mama yake lazima auawe.
16Yeyote atakaye mteka mtu na kumuuza, au mtu amekutwa kama mali yake, huyo mtekaji lazima auawe.
17Yeyote atakaye mlaani baba au mama yake lazima auawe.
18Kama wanaume watapigana na mmoja akimpiga mwengine kwa jiwe au ngumi, na huyo mtu asife, lakini alazwe kitandani;
19kisha akapona na anaweza kutembea kwa gongo lake, yeye aliye mpiga lazima alipe muda aliye mpotezea; na lazima alipe matibabu yake yote. Lakini huyo mtu hana hatia ya mauaji.
20Kama mwanaume akimpiga mtumishi wake wa kiume au wa kike kwa gongo, na kama mtumishi huyo akifa kwa madhara ya pigo, kisha huyo mtu lazima ahadhibiwe.