Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Kutoka

Kutoka 39

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Na kutokana na ule uzi wa bluu na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kitambaa chenye rangi nyekundu ya kochinili wakafanya mavazi yaliyofumwa kwa ajili ya kuhudumu katika mahali patakatifu. Basi wakafanya yale mavazi matakatifu yaliyokuwa kwa ajili ya Aruni, kama vile Yahweh alivyokuwa amemwamuru Musa.
2Basi akaifanya ile naivera ya dhahabu, uzi wa bluu na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kitambaa chenye rangi nyekundu ya kochinili na kitani bora kilichosokotwa.
3Kisha wakafua mabamba ya dhahabu yawe mabamba membamba, naye akakata nyuzi za kufuma pamoja na ule uzi wa bluu na ile sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kile kitambaa chenye rangi nyekundu ya kochinili na kile kitani bora, kama kazi ya mjenzi.
4Wakaifanyia vipande vya begani vilivyounganishwa. Iliunganishwa kwenye miisho yake miwili.
5Nao mshipi, uliokuwa juu yake ili kuifunga, ulikuwa wa kitambaa kilekile kulingana na ufundi wake, wa dhahabu, uzi wa bluu, na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kitambaa chenye rangi nyekundu ya kochinili na kitani bora kilichosokotwa, kama vile Yahweh alivyokuwa amemwamuru Musa.
6Kisha wakafanya mawe ya shohamu yaliyopangwa kwenye mapambo ya dhahabu, yaliyochongwa kwa michoro ya muhuri kulingana na majina ya wana wa Israeli.
7Bezaleli akayaweka kwenye vile vipande vya begani vya naivera yawe mawe ya ukumbusho kwa ajili ya wana wa Israeli, kama vile Yehova alivyokuwa amemwamuru Musa.
8Kisha akafanya kile kifuko cha kifuani kwa ufundi wa mjenzi, kama ule ufundi wa naivera, kutokana na dhahabu, uzi wa bluu na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kitambaa chenye rangi nyekundu ya kochinili na kitani bora kilichosokotwa.
9Kilikuwa mraba kilipokunjwa. Walikifanya kile kifuko cha kifuani, kinapokunjwa, shubiri moja urefu wake na shubiri moja upana wake.
10Kisha wakakijaza kwa mistari minne ya mawe. Mstari wa zabarijadi, topazi na zumaridi ulikuwa mstari wa kwanza.
11Nao mstari wa pili ulikuwa feruzi, yakuti na yaspi.
12Nao mstari wa tatu ulikuwa jiwe la leshemi, akiki na amethisti.
13Nao mstari wa nne ulikuwa krisolito na shohamu na yashefi. Yaliwekwa katika mapambo ya dhahabu katika mahali pake.
14Na mawe hayo yalikuwa kulingana na majina ya wana wa Israeli. Yalikuwa kumi na mawili kulingana na majina yao, kwa michongo ya muhuri, kila moja kulingana na jina lake kwa ajili ya yale makabila kumi na mawili.
15Nao wakafanya juu ya kile kifuko cha kifuani minyororo yenye mashada, msokoto wa kamba, wa dhahabu safi.
16Kisha wakafanya mapambo mawili ya dhahabu na pete mbili za dhahabu na kuziweka hizo pete mbili kwenye ile miisho miwili ya kile kifuko cha kifuani.
17Baada ya hilo wakapitisha zile kamba mbili za dhahabu kwenye zile pete mbili zilizo kwenye miisho ya kile kifuko cha kifuani.
18Nao wakapitisha ile miisho miwili ya zile kamba mbili kwenye yale mapambo mawili. Halafu wakaiweka juu ya vile vipande vya begani vya naivera, mbele yake.

19Kisha wakafanya pete mbili za dhahabu na kuziweka kwenye ile miisho miwili ya kile kifuko cha kifuani kwenye upindo wake ulio upande unaoelekea ile efodi upande wa ndani.
20Halafu wakafanya pete mbili za dhahabu na kuziweka juu ya vile vipande viwili vya begani vya efodi upande wake wa chini, sehemu yake ya mbele, karibu na mahali pake pa kuungania, juu ya ule mshipi wa naivera.
21Mwishowe wakakifunga kile kifuko cha kifuani kwa pete zake kwenye zile pete za efodi kwa uzi wa bluu, ili kipate kuwa juu ya mshipi wa efodi na kile kifuko cha kifuani kisiondoke juu ya efodi, kama vile Yahweh alivyokuwa amemwamuru Musa.
22Bezaleli akafanya lile koti la naivera, lote la uzi wa zambarau, kazi ya mshonaji.
23Na sehemu wazi ya hilo koti ilikuwa katikati yake, kama sehemu wazi ya vazi la chuma. Sehemu hiyo iliyo wazi ilikuwa na ukingo kuizunguka pande zote ili isiraruke.
24Halafu wakafanya kwenye upindo wa hilo koti makomamanga ya uzi wa bluu na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kitambaa chenye rangi nyekundu ya kochinili, vilivyosokotwa pamoja.
25Wakafanya kengele za dhahabu safi na kuziweka kengele hizo katikati ya makomamanga kwenye upindo wa lile koti kuzunguka pande zote, katikati ya makomamanga;
26kengele na komamanga, kengele na komamanga kwenye upindo wa hilo koti kuzunguka pande zote, kwa ajili ya kuhudumu, kama vile Yahweh alivyokuwa amemwamuru Musa.
27Kisha wakafanya zile kamba za kitani bora, kwa ajili ya Haruni na wanawe.
28Na kile kilemba cha kitani bora na yale mavalio ya kichwani ya mapambo ya kitani bora na zile suruali za kitani bora kilichosokotwa,
29na ule ukumbuu wa kitani bora kilichosokotwa na uzi wa bluu na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kitambaa chenye rangi nyekundu ya kochinili, kazi ya mfumaji, kama vile Yahweh alivyokuwa amemwamuru Musa.
30Mwishowe wakafanya lile bamba linalong’aa, ishara takatifu ya wakfu, kutokana na dhahabu safi na kuandika juu yake maandishi kwa mchongo wa muhuri: “Utakatifu kwa Yahweh.”
31Kisha wakalitia uzi wa bluu ili waliweke juu ya kile kilemba upande wa juu. Kama vile Yahweh alivyokuwa amemwamuru Musa.
32Basi kazi ya ile maskani ya hema la mkutano ikafikia mwisho wake. Kwa maana wana wa Israeli waliendelea kufanya kulingana na yote ambayo Yahweh alikuwa amemwamuru Musa.
33Nao wakaileta maskani kwa Musa, lile hema pamoja na vyombo vyake vyote, kulabu zake, viunzi vyake vya mbao, miti yake na nguzo zake na vikalio vyake,
34na kifuniko chake cha ngozi za kondoo-dume zilizotiwa rangi nyekundu na kifuniko chake cha ngozi za sili na pazia la kisitiri,
35na sanduku la ushuhuda na miti yake na kifuniko.
36Wakaleta meza, vyombo vyake vyote, na ule mkate wa wonyesho,

37kile kinara cha taa cha dhahabu safi, taa zake, ule mstari wa taa, na vyombo vyake vyote na yale mafuta ya kuangazia taa,
38na madhabahu ya dhahabu na yale mafuta yanayotumiwa kutia mafuta na ule uvumba uliotiwa manukato na kile kisitiri kwa ajili ya mwingilio wa hema,
39ile madhabahu ya shaba na kile kiunzi chake cha shaba, miti yake na vyombo vyake vyote, ile beseni na kinara chake,
40Wakaleta mapazia ya ua, nguzo zake na vikalio vyake na kile kisitiri kwa ajili ya lango la ua, kamba zake za hema na misumari yake ya hema na vyombo vyote kwa ajili ya utumishi wa maskani, kwa ajili ya hema ya kukutania.
41Wakaleta yale mavazi yaliyofumwa kwa ajili ya kuhudumu katika patakatifu, yale mavazi matakatifu kwa ajili ya Aruni kuhani na mavazi ya wanawe ya kutumikia wakiwa makuhani.
42Kulingana na yote ambayo Yahweh alikuwa amemwamuru Musa, hivyo ndivyo wana wa Israeli walivyoufanya utumishi wote.
43Naye Musa akaiona ile kazi yote, na, tazama, walikuwa wameifanya kama vile Yahweh alivyokuwa ameamuru. Hivyo ndivyo walivyokuwa wamefanya. Basi Musa akawabariki.