1Musa akajibu, “Lakini itakuwaje wasiponiamini mimi au wasiponisikiliza na kusema, 'Yahwe hajakutokea wewe?”
2Yahwe akamwambia, “Hicho ni nini mkononi mwako?” Musa aksema, “Ni fimbo.”
3Yahwe akasema, “Itupe chini.” Musa akaitupa chini ile fimbo, nayo ikageuka na kuwa nyoka. Musa akarudi nyumba.
4Yahwe akamwambia Musa, “Mchukue kwa kumshikia mkia wake.” Hivyo alimchukua yule nyoka. Mara ikaggeuka na kuwa fimbo mkononi mwake tena.
5“Hii ni ili wapate kuamini ya kuwa Yahwe, Mungu wa baba zao, Mungu wa wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo amekutokea wewe.”
6Yahwe pia alimwambia, “Sasaingiza mkono wako ndani ya vazi lako.” Hivyo Musa akaingiza mkono wake ndani ya vazi lake. Na alipoutoa nje, tazama, mkono wake ulikuwa na ukoma, mweupe kama theluji.
7Yahwe akasema, “Ingiza mkono wako ndani ya vazi lako tena.” Hivyo akaingiza mkono wake ndani ya vazi lake, na alipoutoa nje aliona ukiwa mzima tena kama ulivyo mwili wake wote.
8Yahwe akasema, “Kama hawatakuamini wewe - kama hawatazingatia ishara yanggu ya kwanza ya nguvu zangu au kuziamini, basi wataamini ishara ya pili.
9Na ikiwa hawataamini hata ishara hizi zote mbili za nguvu zangu, au wasipokusikiliza wewe, basi chota maji kutoka katika mto na uyamwage katika nchi kavu. Maji utakayoyamwaga yatakuwa damu katika nchi kavu.”
10Ndipo Musa akamwambia Yahwe, “Bwana, mimi ni mzuri wa kuongea, si hapo kwanza au hata baada ya kuwa umeongea na mtumishi wako. Mimi ni mdhaifu wa kuongea na nina kigugumizi.”
11Yahwe akamwambia, “Ni nani anayeumba mdomo wa mwanadamu? Ni nani amfanyaye mwanadamu kuwa bubu au aone au kipofu? Je si mimi Yahwe?
12Sasa nenda, nami nitauongoza mdomo wako na nitakufundisha cha kusema.”
13Lakini Musa akasema, “Bwana, tafadhali mtume mtu mwingine, yeyote unayependa kumtuma.”
14Kisha Yahwe akamkasirikia Musa. Akasema, “Vipi kuhusu Aroni kaka yako yule Mlawi? Najua ya kuwa anaweza kuongea vizuri. Hata hivyo, anakuja kukutana na wewe, na atakapokuona moyo wake utajawa na furaha.
15Wewe utaongea naye na utaweka maneno ya kusema kinywani mwake. Nami nitakiongoza kinywa chako na kinywa chake pia, nami nitaonesha ninyi nyote yawapasayo kutenda.
16Yeye ataongea na watu kwa niaba yako. Yeye atakuwa msemaji wako, na wewe utakuwa kama Mungu kwake.
17Utachukua hii fimbo pamoja nawe mkononi mwako. Kwa fimbo hii utafanya ishara.”
18Hivyo Musa alirudi kwa Yethro - baba mkwe wake na kumwambia, “Niruhusu nipate kurudi kwa ndugu zangu walioko Misri ili niweze kuona kama bado wako hai.” Yethro akwambia Musa, “Nenda kwa amani.”
19Yahwe akamwambia Musa kule Midiani, “Nenda, rudi Misri, kwa kuwa watu wote waliotaka kukuua wameshakufa.”
20Musa akamchukua mke wake na watoto wake wa kiume na kuwapandisha kwenye punda. Akarudi mpaka nchi ya Misri, naye alichukua fimbo ya Mungu pamoja naye mkononi mwake.
21Yahwe akamwambia Musa, “Utakaporudi Misri, jitahidi kufanya ishara zote nilizokupa kufanya mbele ya Farao. Lakini nitaufanya moyo wake kuwa mgumu, naye hawatawaacha watu waende.
22Lazima umwambie Farao, 'Hivi ndivyo asemavyo Yahwe: Israeli ni mtoto wangu, mzaliwa wa kwanza wangu,
23nami nakuamuru, “Mwache mwanangu aende ili apate kuniabudu mimi.” Lakini kwa kuwa umekataa kumwachia, hakika nitamuua mtoto wako wa kiume, mzaliwa wa kwanza wako.”'
24Sasa wakiwa njiani, wakati wa usiku walipopumzika, Yahwe alikutana na Musa na kutaka kumuua.
25Kisha Zipora akachukua kisu kikali na kukata govi la mtoto wake wa kiume na kuligusisha miguuni pake. Kisha akasema, “Hakika wewe ni bwana harusi wangu kwa njia ya damu.”
26Hivyo Yahwe akamwachia. Akasema, “Wewe ni bwana harusi wa damu” kwa sababu ya kutahiriwa.
27Yahwe akamwambia Aroni, “Nenda nyikani ukutane na Musa.” Aroni akaenda na kukutana naye katika mlima wa Mungu, na kumbusu.
28Musa akwambia Aroni maneno yote ya Yahwe ambayo alimtuma kusema na kwa habari za ishara zote za nguvu za Yahwe ambazo alimwagiza kutenda.
29Kisha Musa na Aroni wakaenda na kuwakusanya wazee wote wa Israeli.
30Aroni akawaambia maneno yote ambayo Yahwe alimwambia Musa. Pia alionesha ishara na miujiza ya nguvu za Yahwe mbele ya watu.
31Watu waliamini. Waliposikia ya kuwa Yahwe aliwaona Waisraeli na ya kwamba aliyaona mateso yao, waliinamisha vichwa vyao na kumwabudu.