Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Kutoka

Kutoka 2

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Sasa mwanamme wa kabila la Lawi alimuoa mwanamke Mlawi.
2Yule mwanamke akapata mimba na kuzaa mtoto wa kiume. Alipoona ya kuwa alikuwa mtoto mwenye afaya, alimficha kwa miezi mitatu.
3Lakini alipokuwa hawezi kuendelea kumficha tena, alichukua kikapu cha manyasi akakipaka sifa na lami. Akamtia mtoto ndani yake na kukiweka juu ya maji katika majani kando ya mto.
4Dada yake akasimama kwa mbali ili ajue yatakayompata.
5Binti Farao akashuka kuoga mtoni wakati vijakazi wake wakitembea kando ya mto. Naye akaona kile kikapu katika majani na akamtuma kijakazi wake kwenda kukileta.
6Alipokifungua, aliomwona mtoto. Tazama, mtoto alikuwa analia. Alimhurumia na kusema, “Bila shaka huyu ni mmoja wapo wa watoto wa Waebrania.”
7Basi dada wa yule mtoto akamwambia binti Farao, “Je naweza kwenda kukutafutia mwanamke wa Kiebrania aje akulele mtoto kwa ajili yako?”
8Binti Farao akamwambia, “Nenda.” Hivyo yule binti akaenda na kumwita mama yake yule mtoto.
9Binti Farao akamwambia mama yake yule mtoto, “Mchukue mtoto huyu ukaninyonyeshee, nami nitakupa posho.” Hivyo yule mwanamke akamchukua mtoto na kumnyonyesha.
10Mtoto alipokuwa mkubwa, akamleta kwa binti Farao, na akawa mtoto wake. Akamwita jina lake Musa akisema, “Kwa sababu nilimtoa katika maji.”
11Musa alipokuwa mtu mzima, alienda kwa watu wake na kuona kazi ngumu walizokuwa wanafanya. Alimuona Mmisri akimpiga Mwebrania, mmoja wa watu wa jamii yake.
12Aliangalia huku na kule, na alipoona ya kuwa hakuna mtu, alimuua yule mmisri na kuuficha mwili wake katika mchanga.
13Alienda tena siku iliyofuata, na tazama, Waebrania wawili walikuwa wanapigana. Alimwambia yule aliyekuwa na makosa, “Kwa nini unampigia mwenzako?”
14Lakini yule mtu alisema, “Ni nani aliyekuweka wewe kuwa kiongozi na mwamuzi juu yetu? Unataka kuniua na mimi kama ulivyomuua yule mmisri?” Ndipo Musa akaogopa na kusema, “Hakika niliyoyafanya yamejulikana.”
15Farao aliposikia habari hizi, alijaribu kumuua Musa. Lakini Musa alikimbia na kwenda kuishi katika nchi ya Wamidiani. Kule alikaa chini kando ya mto.
16Wakati huo kuhani wa Midiani alikuwa na mabinti saba. Walikuja mtoni kuchota maji na kujaza vyombo vyao ili wawanyweshe mifuko ya baba yao.
17Wachungaji walikuja na kutaka kuwafukuza, lakini Musa alienda kuwasaidia. Kisha akawanywesha mifugo wao.
18Wale mabinti walipoenda kwa Reueli baba yao, aliwauliza, “Kwa nini mmerudi nyumbani mapema hivi leo?”

19Wakamwambia, “Mmisri mmoja alituokoa dhidi ya wachungaji. Pia alichota maji na kuwanywesha mifugo wetu.”
20Kisha akawauliza binti zake, “Yu wapi sasa? Kwa nini mlimwacha? Mwiteni ili apate kula chakula pamoja nasi.”
21Musa akakubali kukaa na yule mtu ambaye pia alimpa binti yake Zipora ili amuoe.
22Alizaa mtoto wa kiume, na Musa akamwita jina lake Geshomu; akisema; “Nimekuwa mkazi katika nchi ya ugeni.”
23Muda mrefu baadaye, mfalme wa Misri akafa. Waisraeli walilalamika kwa sababu ya kazi za utumwa. Walilia kutafuta msaada, na maombi yao yakamfikia Mungu kwa sababu ya mateso yao.
24Mungu aliposikia malalamiko yao, Mungu alikumbuka agano lake na Abrahamu, na Isaka, na Yakobo.
25Mungu aliwaona Waisraeli na akaielewa hali yao.