Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Sefania

Sefania 3

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Ole kwa mji ulioasi! Mji wenye vurugu umenajisiwa.
2Haukuisikiliza sauti ya Mungu, wala haukupokea masahihisho kutoka kwa Yahwe. Hakumtumaini Yahwe na hatamkaribia Mungu wake.
3Wafalme wao ni simba wanaounguruma miongoni mwao. Waamuzi wao ni mbwa mwitu wa jioni wasiobakiza kitu ambacho kitakuwa kimemung'unywa asubuhi yake.
4Manabii wake wanakiburi na wanaume wasaliti. Makuhani wake wamepanajisi mahali patakatifu na wameifanyia vurugu sheria.
5Yahwe ni mwenye haki miongoni mwao. Hawezi kufanya makosa. Kila asubuhi husimamia haki yake! Haitafichika nuruni, hata hivyo watu wasio wenye haki hawajui kuona aibu.
6Nimeyaharibu mataifa; ngome zao zimeharibiwa. Nimeifanya mitaa yao magofu, hivyo hakuna hata mmoja anayepitia kwake. Miji yao imeharibiwa kwa hiyo hakuna mtu anayeikaa.
7Nikasema, 'Hakika mtaniogopa mimi. Pokeeni masahihisho na msikatiliwe mbali kutoka kwenye miji yenu kwa yote yale niliyokuwa nimeyapanga kuyafanya kwenu.' Lakini walikuwa na shauku kuanza kila siku kwa kuharibu matendo yao yote.
8Kwa hiyo ningojeni - hili ni tamko la Yahwe - mpaka siku ambayo nitainuka kwa ajili ya waathirika. Uaamuzi wangu nikuwakusanya mataifa, kuzikusanya falme, na kumwaga juu yao hasira yangu, uchungu wangu wote mkali, hivyo nchi yote itamezwa kwa moto wa hasira yangu.
9Ndipo nitawapa midomo safi watu, kuwaita wote kwa jina la Bwana kunitumikia wakisimama bega kwa bega.
10Kutoka ng'ambo ya mto Ethiopia waniabuduo - watu wangu waliotawanyika - wataleta dhabihu kwa sababu yangu.
11Katika siku hiyo hamtawekwa kwenye woga kwa matendo yenu yote ambayo mmeyafanya dhidi yangu, tangu wakati ule nitaondoa kutoka kwenu wale waliosherehekea fahari yenu, na kwa sababu hamtakuwa na muda mrefu kufanya majivuno juu ya mlima wangu mtakatifu.
12Lakini nitawaacha kama wa chini zaidi na watu masikini, na mtapata kimbilio katika jina la Yahwe.
13Mkazi wa Israeli si muda mrefu hatafanya udhalimu au kusema uongo, na hakuna ulimi wa udanganyifu utakaoonekana mdomoni mwao; hivyo watalisha na kulala chini, na hakuna hata mmoja atakayewafanya kuogopa.”
14Imba, binti Sayuni! Piga kelele, Israeli. Ufurahi na kushangilia kwa moyo wako wote, binti wa Yerusalemu.
15Yahwe ameiondoa hukumu yako; amewafukuzia mbali adui zako! Yahwe ni mfalme wa Israeli miongoni mwenu. Kamwe hamtamwogopa tena mwovu!.
16Katika siku hizo watasema kwa Yerusalemi, “Usiogope, Sayuni. Usiiache mikono yako ilegee.
17Yahwe Mungu wako yuko katikati yenu, mwenye nguvu wa kuwaokoa. Atasherehekea juu yenu na kwa furaha atakuwa kimya juu yenu kwa upendo wake. Atakuwa na furaha juu yenu na atashangilia kwa furaha,
18katika siku maalumu ya sherehe. Nitaondoa maafa kutoka kwenu; si muda mrefu hamtabeba aibu kwa ajili yake.

19Tazama, Niko tayari kuwashughulikia watesi wenu wote. Katika wakati ule, Nitawaokoa waliolemaa na kuwakusanya waliotupiliwa mbali. Nitawafanya kuwa sifa, na nitaibadilisha aibu yao iwe sifa katika dunia yote.
20Katika wakati ule nitawaongoza; katika wakati ule nitawakusanya pamoja. Nitawafanya mataifa yote ya dunia kuwaheshimu na kuwasifu, wakati mtakapoona hivyo, Nitakuwa nimewarudisha”, asema Yahwe.