Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Sefania

Sefania 2

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Kusanyikeni pamoja ninyi wenyewe mkutano wa hadhara na kusanyikeni, taifa lisilokuwa na aibu -
2kabla amri kuchukua madhara na siku hiyo kupita kama makapi, kabla hasira kali ya ghadhabu ya Yahwe kuja juu yenu, kabla siku ya ghadhabu ya Bwana kuja juu yenu.
3Mtafuteni Yahwe, ninyi watu wote wanyenyekevu duniani mnaozitii amri zake! Tafuteni haki yake. Tafuteni unyenyekevu, na labda mtalindwa katika siku ya ghadhabu ya Yahwe.
4hivyo Gaza utatelekezwa, na Ashkeloni utageuka kuwa uharibifu. Watauondoshea mbali Ashdodi wakati wa mchana, na wataung'oa Ekroni!.
5Ole kwa wanaokaa kando ya bahari, taifa la Wakerethi! Yahwe amesema dhidi yenu, Kanaani, nchi ya Wafilisiti. Nitawaangamiza hakuna mkazi atakayebakia.
6Hiyo nchi ya kando ya bahari itakuwa malisho kwa wachungaji na kwa mazizi ya kondoo.
7Nchi ya kando ya bahari itakuwa mali ya mabaki ya watu wa nyumba ya Yuda, watakaochungia makundi yao huko. Watu wao watalala jioni katika nyumba ya Ashikeloni, kwa kuwa Yahwe Mungu wao atawatunza na kurejesha wafungwa wao.
8Nilizisikia dhihaka za Moabu na wakiwatukana watu wa Amoni wakati walipowadhihaki watu wangu na kujitukuza mipakani mwao.
9Kwa hiyo, kama ninavyoishi - hili ni tamko la Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, - Moabu itakuja kuwa kama Sodoma, na watu wa Amoni kama Gomora; mahali pa viwavi na shimo la chumvi, jangwa la daima. Lakini watu wangu waliosalia watawateka mateka, na watu wa taifa langu waliobaki watachukua umiliki wao.'
10Hili litatokea kwa Moabu na Amoni kwa sababu ya kiburi chao, tangu walipowadhihaki na kuwatukana watu wa Yahwe wa majeshi.
11Ndipo watamwogopa Yahwe, kwa kuwa ataidhihaki miungu yote ya dunia. Kila mmoja atamwabudu yeye, kila mmoja kutoka mahali pake, kutoka kila upande wa pwani.
12Ninyi Wakushi pia mtakufa kwa upanga wangu,
13na mkono wa Mungu utaishambulia kaskazini na kuiangamiza Ashuru, Kwa hiyo Ninawi utatelekezwa kwa kuteketezwa, kuwa pakavu kama jangwa.
14Ndipo makundi ya wanyama yatalala pale, kila mnyama wa mataifa, wote kirukanjia na nungunungu watapumzika juu ya safu zao. Sauti itasikika kutoka madirishani; kifusi kitakuwa milangoni; nakshi za mwerezi wao mihimili itakuwa imeifunua.
15huu ni mji wa kushangiliwa ambao umekaa pasipo hofu, ambaye husema moyoni mwake, “Mimi niko, na hakuna mwingine wa kufanana na Mimi”. Kwa namna ulivyokuwa wa kutisha, mahali pa kulala wanyama ndani yake. Kila mmoja ambaye hupitia kwake huuhisia na kutingisha ngumi kwake.