Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Matendo ya Mitume - Matendo ya Mitume 21

Matendo ya Mitume 21:7-22

Help us?
Click on verse(s) to share them!
7Hata tulipomaliza safari yetu kutoka Tiro, tukafika Tolemai. Pale tulisalimia ndugu, na kukakaa nao kwa siku moja.
8Kesho yake tuliondoka tukaenda Kaisaria. Sisi tukaingia nyumbani mwa Filipo, mhubiri wa injili, aliyekuwa mmoja wa wale saba, nasi tukakaa pamoja naye.
9Mtu huyu alikuwa na mabinti wanne mabikira ambao walitabiri.
10Baada ya kukaa huko kwa siku kadhaa, akashuka kutoka Uyahudi nabii mmoja aitwaye Agabo.
11Yeye alikuja kwetu na akautwaa mkanda wa Paulo. kwa huo alijifunga miguu na mikono yake mwenyewe na kusema, “Roho Mtakatifu asema hivi,” “Wayahudi wa Yerusalemu watamfunga mtu anayemiliki mkanda huu, nao watamkabidhi mikononi mwa watu wa mataifa.”
12Tuliposikia mambo hayo, sisi na watu waliokuwa wakiishi mahali pale tulimsihi Paulo asipande kwende Yerusalemu.
13Ndipo Paulo alijibu, “Mnafanya nini, mnalia na kunivunja moyo wangu? Kwa maana niko tayari, siyo tu kufungwa, lakini pia kufia huko Yerusalemu kwa ajili ya jina la Bwana Yesu.”
14Kwa vile Paulo hakutaka kushawishiwa, tuliacha na kusema, “Basi mapenzi ya Bwana yafanyike.”
15Baada ya siku hizi, tulichukua mifuko yetu na tukapanda Yerusalemu.
16Baadhi ya wanafunzi kutoka Kaisaria pia walifuatana nasi. Wakamleta mtu mmoja aitwaye Mnasoni, mtu wa Kipro, mwanafunzi wa zamani, ambaye tulikaa naye.
17Tulipofika Yerusalemu, ndugu walitukaribisha kwa furaha.
18Kesho yake Paulo alienda pamoja nasi kwa Yakobo, na wazee wote walikuwepo.
19Baada ya kuwasalimu, aliwapa taarifa moja baada ya nyingine ya mambo ambayo Mungu aliyotenda miongoni mwa mataifa kwa kupitia huduma yake.
20Wakati waliposikia hayo, wakamsifu Mungu, na wakamwambia, “Unaona, ndugu, kuna maelfu wangapi wameamini miongoni mwa Wayahudi. Wao wote wana nia ya kushika sheria.
21Wameambiwa kuhusu wewe, kwamba unafundisha Wayahudi wanaoishi kati ya mataifa kuachana na Musa, na kwamba unawaambia wasiwatahiri watoto wao, na wasifuate desturi za zamani.
22Tunapaswa tufanye nini? Bila shaka watasikia kwamba wewe umekuja.

Read Matendo ya Mitume 21Matendo ya Mitume 21
Compare Matendo ya Mitume 21:7-22Matendo ya Mitume 21:7-22