21Watazijenga nyumba na kukaa huko, na watapanda mizabibu na kula matunda yake.
22Hawatajenga nyumba na wengine waishi humo; hawatapanda, na wengine wale; maana kama siku za miti zitakuwa siku za watu wangu. Watu wangu wataishi kikamilifu kwa kazi ya mikono yao.
23Hawatafanya kazi bure, wala kuzaa kwa kusikitishwa. Maana ni watoto wa waliobarikiwa na Yahwe, pamoj na koo zao.
24Kabla hawajaita, nitaitika; na wakati wanaendele kuzungumza, ntisikia. Mbwa mwitu na kondoo watachungwa pamoja, na simba atakula majani kama ng'ombe; lakini udongo utakuwa chakula cha nyoka.