Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Hesabu - Hesabu 22

Hesabu 22:36-41

Help us?
Click on verse(s) to share them!
36Balaki aliposikia kuwa Balaamu alikuwa amekuja, alienda kukutana naye kule mjini Moabu pale Amoni, ambao uko mpakani.
37Balaki akamwambia Balaamu, “Je, mimi sikutuma watu kukuita? Basi kwa nini hukuja kwangu? Je, mimi sina uwezo wa kukufanya uheshimike?”
38Ndipo Balaamu alipomjibu Balaki, “Tazama, mimi nimekuja kwako. Je mimi sina mamlaka ya kusema chochote? Mimi ninaweza kusema maneno ambayo Mungu ameweka kinywani mwangu.”
39Balaamu akaenda na Balaki, na Wakafika Kiriathi Huzothi.
40Kisha Balaki akatoa sadaka ya maksai na kondoo na kumpatia Balaamu baadhi ya hiyo nyama na wale viongozi waliokuwa pamoja naye.
41Kesho yake asubuhi, Balaki akampeleka Balaamu mpaka juu mahali pa Baali. Kule juu Balaamu aliweza kuona sehemu tu ya kambi za Waisraeli.

Read Hesabu 22Hesabu 22
Compare Hesabu 22:36-41Hesabu 22:36-41