Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Amosi

Amosi 9

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Nilimwona Bwana amesimama karibu na madhabahu, na akasema, “Vipige vichwa vya nguzo ili kwamba misingi itikisike. Vivunje vipande vipande juu ya vichwa vyao vyote, nami nitamwua kwa upanga wa mwisho wao. Hakuna hata mmoja wao atakaye kimbia, hakuna hata mmoja wao atakayekimbia. Hata kama watachimba kwenye Sheoli, kuna mkono wangu utawachukua.
2Hata kama watapanda juu kwenda mbingunu, huko nitawaleta chini.
3Hata kama watajificha juu ya Karmeli, nitawatafuta huko na kuwachukua. Hata kama watajificha kwenye vilindi vya bahari nisiwaone, nimwagiza joka, na atawang'ata.
4Hata kama wataenda kwenye utumwa, watabanwa na maadui zao mbele yao, nitauagiza upanga huko, na utawau. Nitaelekeza macho yangu juu yao kwa ubaya sio kwa uzuri.”
5Bwana Mungu wa majeshi ndiye agusaye nchi na ikayeyuka; wote waishio humo wataomboleza; yote yatainuka kama Mto, na itadidimia tena kama mto wa Misri.
6Ni yeye ndiye avijengaye vyumba vyake mbinguni, na kuanzisha kuba yake juu ya dunia. Yeye huita maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya uso wa dunia, Yahwe ndiye jina lake.
7“Je ninyi sio kama watu wa Kushi kwangu, wana wa Israeli? -hivi ndivyo Yahwe asemavyo. Je sikuwapandisha Israeli kutoka nchi ya misri, Wafilisti kutoka Krete, na Washami kutoka Kiri?
8Tazama, macho ya Bwana Yahwe yako juu ya ufalme wenye dhambi, na nitauharibu kutoka kwenye uso wa dunia, isipokuwa kwamba sintoiharibu kabisa nyumba ya Yakobo -hivi ndivyo Yahwe asemavyo.
9Tazama, nitaamuru, na nitaipepeta nyumba ya Israeli miongoni mwa mataifa yote, kama mtu apepetaye ngano kwenye ungo, hivyo basi hakuna hata chembe ya jiwe itakayoanguka kwenye aridhi.
10Watenda dhambi wote katika watu wangu watakufa kwa upanga, wale wasemao, 'Majanga hayatatupita au kukutana nasi.'
11Katika siku hiyo nitainua hema ya Daudi iliyokuwa imeanguka, na kuyafunga matawi yake. Nitayainua magofu yake, na kuijenga tena kama katika siku za zamani,
12Kwamba wamiliki mabaki ya Edomu, na mataifa yote ambayo yameitwa kwa jina langu -hivi ndivyo Yahwe asemavyo-afanyayo haya.
13Tazama, siku zitakuja-hivi ndivyo Yahwe asemavyo-wakati mlimaji atampita mvunaji, na akanyagaye zabibu atampita yeye apandaye mbegu. Milima itadondosha divai tamu, na milima yote itabubujika kwa nayo.
14Nitawarudisha kutoka utumwani watu wangu Israeli. Watajenga magofu ya miji na kuishi humo, watapanda bustani za mizabibu na kunywa divai, na watafanya bustani na kula matunda yao.
15Nitaipanda hadi kwenye nchi yao, na hawataing'oa tena kutoka kwenye nchi ambayo niliyowapatia,” asema Yahwe Mungu wako.