12Ndipo Balaamu alipomjibu Balaki, “Niliwaambia wale wajumbe ulionitumia,
13'Hata kama Balaki atanipa ikulu yake ikiwa imejaa fedha na dhahabu, sitafanya zaidi ya maneno ya BWANA kwa lolote zuri au baya, au kwa chochote ambacho ningetaka kufanya. Ninaweza kusema kile tu ambacho BWANA ananiambia kusema,' Je, sikuwaambia haya?
14Kwa hiyo sasa, tazama, nitarudi kwa watu wangu. Lakini kwanza nikuonye kile ambacho hawa watu watawafanyia watu wako katika siku zijazo.”
15Balaamu alianza unabii huu. Akisema, “Balaamu mwana wa Beori anasema, Mtu yule aliyefumbuliwa macho yake.
16Huu ni unabii wa mtu alisikiaye neno la Mungu, aliye na maarifa toka kwake Yeye aliye juu, aliye na maono kutoka kwa Mwenyezi, Yeye ambaye humpigia magoti macho yakiwa yamefumbuliwa.
17Ninamwona, lakini hayuko hapa sasa. Ninamtazama, lakini siyo karibu. Nyota itatokea katika Yakobo, na fimbp ya enzi itatokea katika Israeli. Naye atawapigapiga viongozi wa Moabu na kuwaharibu wa uzao wa Sethi
18Ndipo Edomu atakapokuwa miliki ya Israeli, na Seiri pia itakuwa milki yao, maadui wa Israeli, ambao Israeli atawashinda kwa nguvu zake.