Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Hesabu - Hesabu 20

Hesabu 20:14-24

Help us?
Click on verse(s) to share them!
14Musa akatuma wajumbe kutoka Kadeshi kwa mfalme wa Edom: Ndugu yako Israeli anasema hivi: “Wewe unajua magumu yote ambayo yametupata.
15Na unajua kuwa babu zetu walienda Misri na waliishi Misri kwa muda mrefu. Wamisri walitutendea vibaya pamoja na babu zetu.
16Tulipomlilia BWANA, akatusikia na kututumia malaika ambaye alitutoa toka Misri. Tazama, sasa tuko Kadeshi, mji unaopakana na nchi yako.
17Tunakuomba uturuhusu kupita katika nchi yako. Hatutapita mashambani wala kwenye mashamba ya mizabibu, wala hatutakunywa maji ya visima vyako. Tutapita kwenye njia kuu ya mfalme. Hatutageuka upande wa kulia wala upande wa kushoto mpaka tutakapopita mpaka wako.”
18Lakini mfalme wa Edomu akamjibu, “Msipite hapa. Kama mtafanya hivyo, Nitakuja na upanga kukuvamia.”
19Ndipo wana wa Israeli wakamwambia, “tutapitia njia kuu. Kama sisi au wanyama wetu watakunywa maji yako, basi tutalipa. Tunaomba uturuhusu tupite tukitembea kwa miguu yetu, bila kufanya jambo lolote lile.”
20Lakini mfalme wa Edomu akajibu, “Usipite hapa.” Kwa hiyo nfalme wa Edomu akawa kinyume cha Israeli kwa mkono wenye nguvu pamoja na jeshi kubwa sana.
21Mfame wa Edomu akawazuia wana wa Israeli kupita kwenye mipaka yake. Kwa sababu ya hili, Israeli akageuka kuiacha nchi ya Edomu.
22Kwa hiyo watu wakasafiri kutoka Kadeshi. Wana wa Israeli, watu wote, wakafika Mlima Hori.
23BWANA akanena na Musa na Haruni hapo kwenye Mlima Hori, kwenye mpaka wa Edomu. Akasema,
24“Sasa ni wakati wa Haruni kukusanyika na watu wake, hataingia katika nchi ile niliyowaahidi wana wa Israeli. Hii ni kwa sababu ninyi wawili hamkuitii sauti yangu pale kwenye maji ya Meriba.

Read Hesabu 20Hesabu 20
Compare Hesabu 20:14-24Hesabu 20:14-24