Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 1Wafalme - 1Wafalme 3

1Wafalme 3:8-16

Help us?
Click on verse(s) to share them!
8Mtumishi wako yuko katikati ya watu wako uliowachagua, kundi kubwa, watu wangi wasiohesabika.
9Kwa hiyo umpe mtumishi wako moyo wa uelewa wa kuwahukumu watu wako. Kwani ni nani awezaye kuwahukumu watu wako hawa walio wengi?”
10Ombi hili la Sulemani likampendeza Bwana.
11Kwa hiyo Mungu akamwambia. “Kwa sababu umeomba jambo hili na haujajiombea maisha marefu au utajiri au uhai wa maadui wako, lakini umeomba ufahamu wa kutambua hukumu ya haki,
12Tazama sasa nitafanya yote uliyoniomba wakati uliponipa ombi lako. Ninakupa moyo wa hekima na ufahamu, kwa kuwa hapajawahi kuwa na mtu wa kuwa kama wewe kabla yako, na hakuna wa kuwa kama wewe atakayeinuka baada yako.
13Pia ninakupa hata ambayo hujaomba, vyote heshima na utajiri, ili kwamba pasije pakawa na mfalme wa kuwa kama wewe katika siku zako zote.
14Kama utatembea katika njia zangu na kuyatunza maagizo yangu na maagizo yangu, kama alivyofanya baba yako Daudi, ndipo nitakapoziongeza siku zako.”
15Kisha Sulemani alipoamka, na tazama, ilikuwa ndoto. Akaja Yerusalemu na akasimama mbele ya sanduku na agano la Bwana. Akatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani, na akawafanyia sherehe watumishi wake wote.
16Kisha wanawake wawili waliokuwa makahaba wakaja mbele ya mfalme wakasimama mbele yake.

Read 1Wafalme 31Wafalme 3
Compare 1Wafalme 3:8-161Wafalme 3:8-16