Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 1Wafalme

1Wafalme 9

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Sulemani alipomaliza kulijenga hekalu la BWANA, na ikulu ya mfalme, na baada ya kukamilisha vyote alivyokusudia kufanya,
2BWANA alionekana kwa Sulemani kwa mara ya pili, kama alivyoonekana kwake kule Gibeoni.
3Na BWANA akamwambia, “Nimeyasikia maombi yako na dua zako ambazo umeniomba. Nimeitakasa nyumba hii ambayo umeijenga, kwa ajili yangu, ili niweke jina langu humo milele. Macho yangu na moyo wangu yatakuwa humo kwa nyakati zote.
4Lakini pia na wewe, kama utatembea mbele zangu kama Daudi baba yako alivyotembea kwa haki na unyofu katika moyo wako, ukitii yote niliyokuamuru na kuyashika maagizo na sheria zangu,
5ndipo nitakapoimarisha kiti cha enzi kwa Israeli milele, kama nilivyomwahidi baba yako Daudi, nikiseama, 'uzao wako hautaondoka katika kiti cha enzi cha Israeli.
6Lakini kama utageuka, wewe au watoto wako, na kutozishika amri zangu na maagizo yangu ambayo nimeyaweka mbele zako, na kama utaenda kuabudu miungu mingine na kuisujidia,
7basi nitaikatilia mbali Israeli kutoka katika ardhi niliyowapa; na nyumba hii niliyoitakasa kwa jina langu, nitaitupilia mbali na macho yangu, na Israeli itakuwa mfano wa kukejeliwa na kitu cha kutusiwa katika mataifa yote.
8Ijapokuwa hekalu hili limetukuka sasa, kila mtu atakayepita pembeni yake atasituka na kuzoomea. Watajiuliza, 'Kwa nini BWANA amefanya hili katika chi hii na kwa nyumba hii?'
9Na wengine watajibu, 'Ni kwa sababu walimwacha BWANA, Mungu wao, ambaye aliwaleta mababu zao toka Misri, na sasa wamegeukia miungu mingine ambayo wameiinamia na kuisujudu. Hiyo ndiyo sababu BWANA amewaletea majanga haya yote.”
10Ilitokea mwishoni mwa miaka ishirini, Sulemani alikuwa amemaliza kuyajenga majengo yote mawili, hekalu la BWANA na ikulu ya mfalme.
11Basi Hiramu, mfalme wa Tiro, alikuwa amemletea Sulemani mbao za mierezi na miboreshi, pamoa na dhahabu; vitu vyote ambavyo Sulemani alitamani. Kwa hiyo mfalme Sulemani akampatia Hiramu miji ishirini huko Galilaya.
12Hiramu akaja kutoka Tiro kuiona ile miji ambayo Sulemani alikuwa amempatia, lakini hakupendezwa nayo.
13Kwa hiyo Hiramu akasema, “Ndugu yangu, ni miji gani hii uliynipatia? Hiramu akaiita nchi ya Kabuli mpaka leo.
14Hiramu alikuwa amemtumia mfalme tani nne za dhahabu.
15Vifuatavyo ndivyo vigezo ambavyo mfalme Sulemani aliweka: ili kulijenga hekalu la BWANA na ikulu yake, kuijenga Milo na ukuta wa Yerusalemu, na Hazori, Megido, na Gezari.
16Farao mfalme wa Misri alikuwa ameenda kuitwaa Gezeri, akaichoma moto, na kuwaua Wakanaani katika mji. Kisha Farao akampatia binti yake ule mji, mke wa Sulemani kuwa zawadi ya arusi.
17Kwa hiyo Sulemani akaijenga Gezeri na Bethi Horoni ya Loweri,
18Baalathi na Tamari jangwani katika nchi ya Yuda,

19na miji yote ya hazina yote iliyokuwa yake, na miji ya magari yake, na miji ya wapanda farasi wake, na hata kama alipenda kuijenga kwa ajili ya fahari yake kule Yerusalemu, Lebanoni, na katika nchi yote kwenye utawala wake.
20Na kwa watu wote waliokuwa wamesalia wa Waamori, Wahiti, Waperezi, Wahivi, na Yebu, ambao hawakuwa Waisraeli,
21na uzao wao waliokuwa wamesalia baada yao katika nchi, ambao Waisraeli hawakuweza kuwaangamiza kabisa - Sulemani akawafanya kuwa vibarua, ambao wako hata leo.
22Hata hivyo, Sulemani hakuwafanya kuwa shokoa watu wa Israeli. Badala yake, walifanyika kuwa wanajeshi wake na watumishi wake, maakida wake, na wakuu wake, na majemedari wake na wapanda farasi wake.
23Hawa ndio waliokuwa maakida wakuu waliokuwa wakiwasimamia kazi za Sulemani, watu 550, walikuwa wasimamizi wa watu waliokuwa wakifanya kazi.
24Binti wa Farao alihama kutoka mji wa Daudi kwenda kwenye ile nyumba ambayo Sulemani alimjengea. Baadaye, Sulemani akaijenga Milo.
25Mara tatu kwa kila mwaka Sulemani alitoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani katika madhabahu ambayo alimjengea BWANA, akifukiza uvumba pamoja nazo juu ya madhabahu ilyokuwa mbele ya BWANA. Kwa hiyo akalimalizia hekalu na sasa alikuwa akilitumia.
26Tena Sulemani alitengeneza merikebu kule Ezioni Geberi, ambayo iko karibu na Elathi katika ufukwe wa bahari ya shamu, katika nchi ya Edomu.
27Hiramu alituma watumishi kwenye merikebu ya Sulemani, wanamaji wanaoijua bahari, pamoja na watumishi wake Sulemani.
28Walikwenda kwa Ofri pamoja na watumishi wa Sulemani. Kutoka huko walileta takribani tani 14. 5 za dhahabu kwa Sulemani.