Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 1Wafalme

1Wafalme 7

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Ilimchukua Sulemani miaka kumi na tatu kujenga ikulu yake.
2Aliijenga ikulu iliyoitwa mwitu wa Lebanoni. Urefu wake ulikuwa mita 46, na upanawake ulikuwa mita 23, na kimo chake kilikuwa mita 14. Nayo ilikuwa na safu nne ya nguzo za mierezi na mithili ya mwerezi juu ya nguzo.
3Paa la ikulu lilikuwa la mwerezi ambalo lilikaa juu ya mihimili. Mihili hiyo ilikuwa imeshikiliwa na nguzo. Kulikuwa na mihimili arobaini na tano, ambayo ilikuwa katika safu kumi na tano.
4Nayo mihimili ilikuwa safu tatu, na kila dirisha lilikabili dirisha lingine katika madaraja matatu.
5Milango yote na miimo ilitengenezwa kwa mraba, na madirisha yalikuwa yakikabiliana katika madaraja matatu
6Akatengeneza baraza lenye uerfu wa mita 23 na upana wa mita 14. Mbele yake kulikuwa na ukumbi ulioezekwa.
7Sulemani akajenga baraza yenye kiti cha enzi ambacho alitolea hukumu ya haki. Nayo ilikuwa imeezekwa kwa mwerezi kutoka sakafu moja hadi nyingine.
8Nyumba ya Sulemani ambayo alikusudia kuishi, katika behewa nyingine ndani ya sehemu ya chini ya ikulu, ilitengenezwa kwa kazi hiyo hiyo. Pia alimjengea binti wa Farao nyumba kama hii, ambaye alikuwa mke wake
9Majengo haya yalipmbwa kwa vitu vya thamaini, mawe ya thamani, yaliyochongwa na kukatwa kwa msimeno kufuata vipimo sahihi na kulainishwa pande zote. Mawe ya namna hii ndiyo yale yaliyotumika kuanzia kwenye msingi hadi juu, pia na nje hadi kwenye baraza.
10Msingi ulijengwa kwa mawe makubwa sana na ya thamani yenye urefu wa mita 3. 7 na mengine mita 4. 8.
11Kwa juu ilipambwa kwa, mawe ya thamani yaliyochongwa sawa sawa kwa msimeno na kwa mihimili ya mierezi.
12Na behewa kubwa iliyokuwa ikizunguka ikulu ilikuwa na safu tatu za mawe yaliyokatwa na safu moja ya mihimili ya mierezi kama ilivyo kwenye baraza la ndani la hekalu la BWANA na ule ukumbi wa hekalu.
13Mfalme Sulemani alituma watu kumleta Huramu kutoka Tiro.
14Huramu alikuwa mwana wa mjane wa kabila ya Naftali; baba yake alikuwa mtu wa Tiro, mfua shaba. Huramu alikuwa mwingi wa hekima na ufahamu na stadi za kufanya kazi kubwa za shaba. Aliletwa kwa mfalme ili kufanya kazi zilizohusiana na shaba kwa mfalme.
15Huramu alizilemba zile nguzo mbili za shaba, kila moja ilikuwa na kimo cha mita 8. 3 na mzingo wa mita 5. 5.
16Akatengeneza taji mbili za shaba za kuwekwa juu ya zile nguzo. Kimo cha kila taji ilikuwa mita 2. 3.
17Kulikuwa na nyavu za kuwa kama kazi ya kusuka, na masongo ya mikufu, kwa ajili ya kuvipamba vile vichwa vya nguzo, nayo yailikuwa saba kwa kila kichwa.
18Kwa hiyo Huramu akafanya safu mbili za komamanga kuzunguka vile vichwa vya nguzo ili kuvipamba vile vichwa.

19Zile taji kwenye vile vichwa vya nguzo za ukumbi zilikuwa zimepambwa kwa maua, yenye vimo vya mita 1. 8.
20Hizo taji kwenye hizo nguzo mbili kwenye vichwa vyake, karibu yake kulikuwa na makomamanga mia mbili yote yakiwa kwenye safu.
21Alisimamisha nguzo kwenye ukumbi wa hekalu. Ile nguzo ya kuume akaipa jina la Yakini, na ile ya kushoto akaipa jina la Boazi.
22Na juu ya zile nguzo kulikuwa na mapambo kama maua. Hivyo ndivyo zile nguzo zilivyotengenezwa.
23Tena akafanya bahari ya kusubu ya, yenye mita 2. 3 kutoka ukingo hadi ukingo, kimo chake kilikuwa mita 4. 6, mziingo wake ulikuwa mita 13. 7.
24Na chini ya ile bahari kulikuwa na vibuyu vilivyoizunguka, vilikuwa vibuyu kumi na nane katika kila mita, vilivyowekwa katika kila hicho kipande wakati bahari inapokuwa kalibu.
25Bahari ikakaa juu ya makisai kumi na mbili, tatu, zilitazama kaskazini, tatu zikitazama magharibi, tatu zikitazama kusini na tatu zikitazama kaskazini. Ile bahari iliwekwa juu yao, na pande zao zote za nyuma zilikuwa ndani.
26Bahari ilikuwa nene kama upana wa mkono, na ukingo wake ulikuwakama ukingo wa kikombe, kama ua la yungi huingia bathi elfu mbili za maji.
27Huramu akatengeneza makalio kumi ya shaba. Kila kalio lilkuwa na urefu wa mita 1. 8, upana wa mita 1. 8, na kimo cha mita 1. 3.
28Hivi ndivyo kazi za makalio zilivyofanywa. Yalikuwa na papi ambazo zilikaa kati kati ya vipandio,
29na juu ya papi na vipandio kulikuwa na simba, makisai, na makerubi. Chini na juu simba kulikuwa na masongo ya kazi ya kufuliwa.
30Kila kalio lilikuwa na magurudumu ya shaba na vipini, na pande zake nne na miguu yake minne ilikuwa na mataruma chini ya birika. Chini ya birika yalikuweko mataruma ya kusubu yenye masongo katika kila upande.
31Na kinywa chake kilikuwa cha kuviringana, chenye upana wa sentimita araobaini na sita, na ile taji ilikuwa na sentimita ishirini na tatu. Na kinywa chake kilikuwa na nakshi, na papi zake zilikuwa za mraba, na wala siyo za mvringo.
32Yale magurudumu mawili yalikuwa chini ya papi, na mikono ya magurudumu yalikuwa ndani ya makalio. Kimo cha yale magurudumu kilikuwa sentimeta sitini na tisa.
33Yale magurudumu yalikuwa kama ya gari. Mikono yake, na maduara, matindi yake, na vipande vya ndani vyote vilikuwa vya kusubu.
34Kulikuwa na mataruma manne katika pande zake nne za makalio, yaliyokuwa yameshikamanishwa na kalio lenyewe.
35Juu ya makalio kulikuwa na duara yenye kina cha sentimita ishirini na tatu, na juu ya makalio mashikio yake na papi zake zikiwa zimeshikamanishwa.
36Juu ya mabamba na papi zake Huramu akachora makerubi, simba, na mitende ambayo ilifunika nafasi ya juu, nayo ilikuwa imezungukwa na masongo.

37Alitengeneza makalio kumi kwa jinsi hii. Yote yalikuwa yametengenezwa kwa kufanana, na yalikuwa ya vipimo sawa, na sura inayofanana.
38Huramu akatengeneza birika kumi za shaba. Birika moja liliweza kubeba bathi arobaini za maji. Kila birika lilikuwa mita 1. 8 toka birika moja hadi jingine na kulikuwa na birika moja katika kila kalio kati ya yale kumi.
39Alitengeneza makalio tano upande wa kusini unaoelekea upande wa hekalu. Akatengeneza bahari katika upande wa mashariki, ukielekea upande wa kusini wa hekalu.
40Huramu akatengeneza birika na koleo na besini la kunyunyizia. Kisha akamaliza kazi yote aliyofanya kwa mfalme Sulemani katika hekalu la BWANA:
41Zile nguzo mbili, na lile besini lakawa kama taji ambalo lilikuwa juu ya zile nguzo, na nyavu mbili za mapambo za kufunika zile besini mbili za kuwa kama taji zilizokuwa juu ya nguzo.
42Kisha akatengeneza makomamanga mia nne kwa ajili ya zile nyavu mbili za mapambo: safu mbili za makomamamanga kwa kila kazi ya nyavu kwa ajili ya kufunikia zile besini mbili kama taji iliyo juu ya nguzo,
43yale makalio kumi, na birika kumi kwenye makalio.
44Akatengeneza bahari na makisai kumi chini yake;
45na masufuria, koleo, birika na vyombo vingine vyote. Huramu akivitengeneza kwa shaba iliyosuguliwa, kwa ajili ya mfalme Sulemani, na kawa ajili ya hekalu la BWANA.
46Mfalme alivisubu katika uwanda wa Yorodani, katika udongo mfinyanzi kati ya Sukoti na Zarethani.
47Sulemani hakuvipima vyombo vyote kwa sababu vilikuwa vingi mno kuvipima, na kwa sababu uzito wa shaba ulikuwa hauwezi kupimwa.
48Sulemani akatengeneza mapambo yote yaliyokuwa kwenye hekalu la BWANA kwa kutumia dhahabu: Ile madhabahu ya dhahabu na ile meza ambayo iliwekwa mikate ya wonyesho.
49Vile vinara vya dhahabu, ambavyo vitano vilikuwa upande wa kulia na vitano mkono wa kushoto, mbele ya chumba cha ndani, vilikuwa vya dhahabu safi, na maua, na taa na koleo zilikuwa za dhahabu.
50Vile vikombe, na makasi, mabakuri, na vijiko, na vyetezo vyote vilikuwa vimetengenezwa kwa dhahabu safi. na bawaba za dhahabu za milango ya ndani, ambazoo ndio mahali patakatifu sana, na milango ya ukumbi mkubwa, vyote vilitengenezwa kwa dhahabu.
51Kwa njia hii, kazi yote ambayo mfalme Sulemani alifanya kwa ajili ya hekalu ilimalizika. Kwa Sulemani akaviingiza ndani yake vitu vile vilivyokuwa vimewekwa wakfu na Daudi, baba yake, na fedha na dhahabu, na mapambo, na vile vya ndani ya hazina ya BWANA.