1Kwa hiyo Sulemani akaanza kulijenga hekalu. Hii ilikuwa mwaka wa 480 baada ya wana wa Israeli kutoka katika nchi ya Misri, katika mwaka wa nne wa utawala wa Sulemani huko Israeli, katika mwezi wa Ziv, ambao ndio mwezi wa pili.
2Hekalu ambalo mfalme Sulemani alimjengea BWANA lilikuwa na urefu wa mita 27, na upana wa mita 9, na kimo cha mita 13. 5.
3Na ukumbi uliokuwa mbele ya hekalu ulikuwa na urefu wa mita 9 na upana wa mita 4. 5 sawa na upana wa sehemu kuu ya hekalu.
4Lile hekalu alilitengenezea madirisha ambayo fremu zake kwa nje yalifanya yaonekane membamba kuliko ile sehemu ya ndani.
5Na ukuta wa nyumba aliuzungushia vyumba kuzunguka pande zake, kushikamana na vyumba vya nje na vya ndani ya hekalu. Akajenga vyumba katika pande zote.
6Kile chumba cha chini kilikuwa na upana wa mita 2. 3, kile cha kati kilikuwa na upana wa mita 2. 8. na kile cha tatu kilikuwa na upana wa mita 3. 2. upande wa nje akaupunguza ukuta wa nyumba pande zote, ili boriti zisishikamane ukutani mwa nyumba.
7Hekalu lilijengwa kwa mawe yaliyokuwa yamechongwa chimboni. Hakuna nyundo, wala shoka au chombo chochote cha chuma kilisikika wakati hekalu lilipokuwa likjengwa.
8Upande wa kusini wa hekalu kulikuwa na lango la chini, ambalo mtu hupanda kwa madaraja mpaka juu kwenye chumba cha kati, na kutoka chumba cha kati hadi chumba cha tatu.
9Kwa hiyo Sulemani akalijenga hekalu mpaka akalimaliza, akalifunika hekalu kwa boriti na mbao za mwerezi.
10Akajenga vyumba vya pembeni mwa hekalu, kila upande mita 2. 3 kwenda juu. Navyo vikaunganishwa na hekalu kwa mbao za mierezi.
11Neno la BWANA likamjia Sulemani, likisema,
12“Kuhusu hili hekalu ambalo unajenga, kama utatatembea katika maagizo yangu na kuhukumu kwa haki, na kutunza amri zangu na kuishi kwa hizo, ndipo ntakapozithibitisha ahadi zangu na wewe ambazo niliziahidi kwa baba yako Daudi.
13Nitaishi kati ya watu wa Israeli nami sitawatupa.”
14Kwa hiyo Sulemani akalijenga hekalu mpaka akalimaliza.
15Kisha akajenga kuta za ndani za hekalu kwa mbao za mwerezi. Kuanzia sakafu ya hekalu hadi boriti za juu, kwa ndani akazifunika kwa miti, na akaifunika sakafu kwa mbao za miberoshi.
16Alijenga mita 9 ndani ya hekalu kwa mbao za miberoshi kutoka sakafuni hadi juu. Hiki ni chumba cha ndani, cha patakatifu sana.
17Ule ukumbu mkuu, ulikuwa mahali pakatifu amabao ulikuwa mbele ya patakatifu sana, ulikuwa wa mita 18. hapo kulikwa na mbao za mwerezi ndani ya hekalu, zilizokuwa zimechongwa kwa sura ya vibuyu na maua yaliyochanua.
18Zote zilikuwa za mierezi kwa ndani. Hapakuonekana chochote ndani kilichokuwa kimetengenezwa kwa mawe.
19Sulemani alitengeneza kile chumba cha ndani kwa lengo la kuweka sanduku la agano la BWANA.
20Kile chumba cha ndani kilikuwa na upana wa mita 9, na kimo cha mita 9. Sulemani alizifunika kuta kwa dhabahu na madhabahu aliifunika kwa mbao za mierezi.
21Sulemani alifunika ndani ya hekalu kwa dhahabu safi na akaweka mikufu ya dhahabu iliyopita mbele ya chumba cha ndani, na kulifunika eneo la mbele kwa dhabahu.
22Akalisakafia kwa dhahabu eneo lote la ndani mpaka akamaliza hekalu lote. Pia akalisakafia kwa dhahabu madhahabu yote ya chumba cha ndani.
23Sulemani akatengeneza makerubi mawili kwa mbao za mizeituni, kila moja lilikuwa na kimo cha mita 4. 5 kwa ajili ya chumba cha ndani.
24Bawa moja la kerubi wa kwanza lilikuwa na urefu wa mita 2. 3. Kwa hiyo kutoka ncha ya bawa moja hadi ncha ya bawa lingine kulikuwa na umbali wa mita 4. 5. Yule
25kerubi mwingine naye alikuwa na bawa lenye kipimo cha mita 4. 5 Makerubi hawa walikuwa wanafanana kwa umbo na kwa vipimo.
26Kimo cha kerubi mmoja kilikuwa mita 4. 5 na yule wa pili alikuwa hivyo hivyo.
27Sulemani aliwaweka hao kerubi kwenye chumba cha patakatifu sana. Bawa moja la kerubi lilikuwa limeenea kiasi kwamba bawa moja liligusa ukuta huu na bawa la yule wa pili nalo liligusa ukuta wa upande mwingine. Hayo mabawa yalikuwa yanakutana katikati ya chumba cha patakatifu sana.
28Sulemani aliwafunika hao kerubi kwa dhahabu.
29Akazinakshi kuta zote kwa sura za makerubi, miti ya mitende, na maua yaliyochanua, kwa vyumba vya nje na vya ndani.
30Sulemani akalisakafia hekalu kwa dhahabu, kwa vyumba vyote vya ndani na vya nje.
31Sulemani akatengeneza milango ya mbao za mizeituni kwenye lango la kuingia ndani. Aliweka vizingiti na miimo kwenye pande tano.
32Kwa hiyo akatengeneza na milango miwili ya mizeituni, na akainakshi kwa makerubi, na mitende, na maua yaliyochanua. Akasakafia kwa dhahabu na akatandaza dhahabu kwenye makerubi na kwenye mitende.
33Kwa njia hii, akalitengenezea hekalu miimo miwili ya mbao za mizeituni yenye pande nne
34na milango miwili ya mbao za mierezi. Zile mbao mbili za mlango mmoja zilikuwa zikijikunja na mbao mbili za mlango wa pili nazo zilikuwa zikijikunja pia.
35Akazinakshi kwa makerubi, mitende, na maua yaliyochanua, na pia akazisakafia kwa dhahabu juu ya zile nakshi.
36Akalijengs Korido la ndani kwa safu tatu za mawe ya kuchongwa na safu moja ya mhimili wa mierezi.
37Msingi wa hekalu ulijengwa katika mwaka wa nne, wa mwezi wa Ziv.
38Mwaka wa kumi na moja mwezi wa Buli, ambao ndio mwezi wa nane, sehemu zote za hekalu zilimalizika na sharti zake zote. Sulemani alilijenga hekalu kwa miaka saba.