Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 1Samweli

1Samweli 14

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Siku moja, Yonathani mwana wa Sauli alimwambia mbeba silaha wake aliye mdogo, “Njoo, hebu twende hadi upande mwingine kwenye ngome ya Wafilisti.” Lakini hakumjulisha baba yake.
2Sauli alikuwa akikaa nje ya mji wa Gibea chini ya mti wa mkomamanga ulio katika Migroni. Takribani watu mia sita walikwa pamoja naye,
3akiwemo Ahiya mwana wa Ahitubu (nduguye Ikabodi) mwana wa Finehasi, mwana wa Eli, kuhani wa BWANA huko Shilo, aliyevaa naivera. Watu hao hawakujua kwamba Yonathani ameondoka.
4Katikati ya vichochoro, ambavyo Yonathani alinuia kuvipita hadi ngome ya Wafilisti, kulikuwa na mwamba wenye mteremko mkali upande mmoja, na mteremko mkali upande mwingine. Jabali moja liliitwa Bosesi, na jingine liliitwa Sene.
5Lile jabali lenye mteremko mkali zaidi liliinuka upande wa kaskazini mbele ya Mikmashi, na jingine upande wa kusini mbele ya Geba.
6Yonathani akamwambia kijana mbeba silaha, “Njoo, na tuvuke hadi ngome ya hawa wasiotahiriwa. Pengine BWANA atatenda kwa niaba yetu, kwa maana hakuna kitu kiwezacho kumzuia BWANA asiokoe kwa wengi au kwa watu wachache.”
7Mbeba silaha wake akajibu, “Fanya kila kitu kilicho ndani ya moyo wako. Songa mbele, tazama, niko pamoja nawe, nitatii maagizo yako yote.”
8Ndipo Yonathani akasema, “Tutavuka twende kwa watu hao, na tutajionesha wenyewe kwao.
9Kama watatuambia, 'Subirini hapo hadi tutakapokuja kwenu' - basi tutabaki katika sehemu yetu na hatutavuka kwenda kwao.
10Lakini kama watajibu, 'Njoni kwetu,' ndipo tutavuka; kwa sababu BWANA amewaweka mkononi mwetu. Hii ndiyo itakuwa ishara yetu.”
11Kwa hiyo wote wawili wakajifunua mbele ya ngome ya Wafilisti. Wafilisti wakasema, “Angalia, Webrania wanakuja kutokea kwenye mashimo walimojificha.”
12Ndipo watu wa ile ngome wakamwita Yonathani na mbeba silaha wake, wakisema, “Njoni huku kwetu, tutawaonesha jambo fulani.” Na Yonathani akamwambia mbeba silaha wake; “Nifuate nyuma yangu, kwa sababu BWANA amewaweka katika mkono wa Israeli.”
13Yonathani alipanda juu kwa mikono na miguu yake, na mbeba silaha akimfuata nyuma yake. Wafilisti waliuwawa mbele ya Yonathani, na mbeba silaha wake akiwaua baadhi nyuma yake.
14Hilo shambulio la kwanza walilofanya Yonathani na mbeba silaha wake, waliua watu wapatao ishirini katika urefu wa nusu handaki kwenye eka moja ya ardhi.
15Kukawa na hofu kubwa katika kambi, uwandani, na katika watu. Hata ngome ya jeshi na watekaji nyara nao wakawa na hofu kubwa
16Ndipo walinzi wa Sauli huko Gibea ya Benyamini wakaona kundi la askari wa Wafilisti likitawanyika, wakienda kule na huku.
17Kisha Sauli akawaambia watu aliokuwa nao, “Mjihesabu ili muone nani hayupo hapa.” Walipokuwa wamehesabu, wakagundua kuwa Yonathani na mbebaji wa silaha zake hawapo.
18Sauli akamwambia Ahiya, “Lete hapa naivera ya Mungu”- kwa maana siku hiyo Ahiya alivaa naivera akiwa pamoja na askari wa Israeli.

19Wakati Sauli akiongea na kuhani, kelele na ghasia kubwa iliendelea na kuongezeka katika kambi ya Wafilisti. dipo sauli akamwambia kuhani, “Acha kazi unayofanya.”
20Sauli na watu wote aliokuwa nao wakajipanga na kwenda kwenye mapigano. Upanga wa kila Mfilisti ulikwa juu ya Mfilisti mwenzake, na kulikuwa na ghasia kubwa.
21Basi Waebrania ambao mwanzoni walijiunga na Wafilisti, na kwenda kwenye kambi yao, wao pia waliungana na Waisraeli waliokuwa pamoja na Sauli na Yonathani.
22Waisraeli wote waliokuwa wamejificha katika milima karibu na Efraimu waliposikia kwamba Wafilisti wamekimbia, nao pia wakawafuata Wafilisti nakuwafukuza kwenye hiyo vita.
23Hivyo siku hiyo BWANA aliwaokoa Israeli, na mapigano yalivuka kupitiliza Beth aveni.
24Siku hiyo watu wa Israeli walifadhaika kwa sababu Sauli aliwaweka watu chini ya kiapo akasema, “Na alaaniwe mtu atakaye kula chakula kabla ya jioni na kabla sijalipiza kisasi kwa maadui zangu.” Hivyo hakuna hata mmoja kati ya watu wote aliyeonja chakula.
25Ndipo watu wote wakaingia msituni na kuona asali ikiwa juu ya ardhi.
26Watu walipoingia humo msituni, asali ilitiririka, lakini hakuna aliyeweka mkono wake kinywani kwa maana watu waliogopa kiapo.
27Lakini Yonathani alikuwa hajasikia kwamba baba yake amewaagiza watu kwa kiapo. Akanyoosha ncha ya fimbo iliyokuwa mkononi mwake na kuichovya kwenye sega la asali. Kisha akanyoosha mkono wake hadi kinywani mwake, na macho yake yakaangaziwa.
28Ndipo mmoja wa watu hao, akamwambia, “Baba yako aliwaagiza watu kwa mkazo na kwa kiapo, kwa kusema, 'Alaaniwe mtu atakaye kula chakula kwa siku ya leo,' ingawa watu wamedhoofika kwa ajili ya njaa.”
29Baadaye Yonathani alisema, “Baba yangu amefanya matatizo katika nchi. Angalia jinsi macho yangu alivyotiwa nuru kwa sababu nilionja asali hii kidogo.
30Je, siyo vivuri sana kama leo watu wangekula bila kizuizi nyara walizopata kutoka kwa maadui zao? Kwa sababu sasa mauaji hayakuwa makubwa katikati ya Wafilisti.”
31Siku hiyo waliwashambulia Wafilisti kutoka Mikmashi hadi Aiyaloni. Na watu walikuwa wamechoka sana.
32Hivyo watu wakazivamia nyara na kuchukua kondoo, ng'ombe na ndama na kuwachinja hapo chini. Watu walikula nyama zao pamoja na damu.
33KIsha wakamwambia Sauli, “Tazama, watu wanamtenda BWANA dhambi kwa kula pamoja na damu.” Sauli akasema, “Mmetenda isivyo haki. Sasa, viringisheni jiwe kubwa kwangu.” Sauli akasema,
34“Nendeni kati watu, na muwaambie, 'Kila mtu alete ng'ombe na kondoo wake, wawachinje hapa, na kuwala. Msimtende BWANA dhambi kwa kula na damu.”' Kwa hiyo watu wote wakaleta kila mtu na ng'ombe wake usiku huo na kuwachinja mahali hapo.
35Sauli akamjengea BWANA madhabahu, ambayo ilikuwa ya kwanza kwake kumjengea BWANA.
36Ndipo Sauli akasema, “Haya tuwafukuze Wafilisti usiku na kuwateka nyara hadi asubuhi; tusimwache hata mtu mmoja akiwa hai.” Nao wakamjibu, “Fanya unaloona linakupendeza.” Lakini kuhani akasema, “Hebu na tumkaribie Mungu mahali hapa.”

37Sauli alitaka kumuuliza Mungu maswali zaidi, “Je, inanipasa kuwafukuza Wafilisti? Je, utawaweka katika mkono wa Israeli?” Lakini siku hiyo BWANA hakumjibu kitu.
38Ndipo Sauli akasema, “Njoni hapa, viongozi wote wa watu; mjue na kuona jinsi dhambi hii ilivyotokea leo.
39Kwa maana, kama BWANA aishivyo, aliyewaokoa Israeli, hata kama angekuwa mwanangu Yonathani, atapaswa kufa.” Lakini hakuna hata mtu mmoja miongoni mwa watu aliye mjibu neno.
40Basi akawaambia Waisraeli wote, “Simameni upande mmoja, na mimi na Yonathani tutasimama upande mwingine.” Kisha watu wakamwambia Sauli, “Fanya lile unaloona jema kwako.”
41Kwa hiyo, Sauli akamwambia BWANA, Mungu wa Israeli, “Tuoneshe Thumimu.” Yonathani na Sauli wakatwaliwa, lakini watu walinusurika kuchaguliwa.
42Basi Sauli akasema, “Tupa mawe ya bahati nasibu tuone kati yangu na mwanangu Yonathani.” Ndipo Yonathani akatwaliwa.
43Kisha Sauli akamwambia Yonathani, “Niambie umefanya nini.” Yonathani akamwambia baba yake, “Nilionja asali kidogo kwa kutumia ncha ya fimbo iliyokuwa mkononi mwangu. Niko hapa; Nitakufa.”
44Sauli akasema, “Mungu afanye hivyo na kuzidi hata kwangu, kama Yonathani hautakufa.”
45Basi watu wakamuuliza Sauli, “Je, inampasa Sauli afe, ni nani aliyetekeleza ushindi huu mkubwa kwa ajili ya Israeli? Mbali na hayo! Kama BWANA aishivyo, hata unywele mmoja wa kichwa chake hautaanguka chini, kwa maana leo amefanya kazi pamoja na Mungu.” Hivyo hao watu walimuokoa Yonathani ili asife.
46Basi Sauli akasita kuwafuatia Wafilisti, nao wakarudi katika makao yao.
47Sauli alipoanza kutawala juu ya Israeli, alipigana na adui zake wote kila upande. Alipigana dhidi ya Moabu, dhidi ya watu wa Amoni, Edomu, wafalme wa Zoba, na Wafilisti. Popote alipogeukia aliwapiga kwa adhabu adui zake.
48Alitenda kwa ushujaa mkubwa na kuwashinda Waamaleki. Aliwaokoa Israeli kutoka mikono ya watu ambao waliwateka nyara.
49Basi wana wa Sauli walikuwa ni hawa Yonathani, Ishvi, na Malkishua. Na majina ya binti zake wawili yalikuwa ni haya, Merabu mzaliwa wa kwanza, na mdogo aliitwa Mikali.
50Jina la mke wa Sauli aliitwa Ahinoamu; naye alikuwa binti Ahimaasi. Na jina la Jemedari wa jeshi lake aliitwa Abneri mwana wa Neri, baba mdogo wa Sauli.
51Kishi alikuwa baba yake Sauli; na Neri alikuwa baba yake na Abneri, wote walikuwa wana wa Abieli.
52Kulikuwa na mapigano makali dhidi ya Wafilisti katika siku zote za Sauli. Naye alipomwona mtu yeyote mwenye nguvu, au mtu yeyote jasiri, alimuunganisha kwake.