Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yoshua - Yoshua 21

Yoshua 21:8-29

Help us?
Click on verse(s) to share them!
8Basi, watu wa Israeli waliwapa Walawi miji hii pamoja na maeneo yao ya kuchungia, kwa kupiga kura, kama vile Yahweh alivyokuwa ameagiza kwa mkono wa Musa.
9Kutoka kwa makabila la Yuda na Simoni, waliwapa nchi katika miji ifuatayo iliyoorodheshwa kwa majina.
10Miji hii walipewa wazawa wa Haruni, ambao walikuwa miongoni mwa koo za Wakohathi, ambao walitoka katika kabila la Lawi. Kwa kuwa upigaji wa kura ya kwanza uliwaangukiwa wao.
11Waisraeli waliwapatia Kiriathi Arba (Arba alikuwa ni baba wa Anaki), eneo hilo liliitwa pia Hebroni, katika nchi ya milima ya Yuda, pamoja na maeneo ya kulishia mifugo yaliyouzunguka mji.
12Lakini mashamba ya mji na vijiji vyake vilikuwa tayari ameshapewa Kalebu mwana Yefune, kama mali yake.
13Na kwa wana wa Haruni kuhani, waliwapa Hebroni pamoja na eneo lake la kulishia mifugo ambao ulikuwa ni mji wa makimbilio kwa mtu aliyeua mtu bila kukusudia na Libna pamoja na maeneo ya kulishia mifugo.
14Na Yatiri pamoaja na maeno yake ya kuchungia, na Eshitemoa pamoja na maeneo yake ya malisho.
15Lakini pia waliwapa Holoni pamoja na maeneo yake ya malisho, Debiri pamoja na maeneo yake ya malisho,
16Aini pampoja na maeneo yake ya malisho, na Bethi Shemeshi pamoja na maeneo yake ya malisho. Ilikuwa ni miji kumi na tisa ambayo walipewa kutoka katika makabila haya mawilil.
17Kutoka katika kabilala Benyamini walipewa Gibea pamoja na maeneo yake ya malisho, na Geba pamoja na maeneo yake ya malisho,
18na Anathothi pamoja na maeneo yake ya malisho, na amoni pamoja na vitongoji vyake vinne.
19Miji waliyopewa makuhani, wana wa Haruni, ilikuwa ni miji kumi na mitatu kwa ujumla, kujumlisha na maeneo yake ya malisho.
20Na kwa ajili ya sehemu ya familia ya Kohathi iliyosalia, wale Walawi walio wa familia ya Kohathi, walipewa miji kutoka katika kabila la Efraimu kwa kupiga kura.
21Walipewa Shekemu pamoja na maeneo yake ya malisho katika nchi ya milima ya Efraimu - mji wa makimbilio kwa mtu aliyeua mtu bila kukusudia, na Gezeri pamoja na maeneo yake ya malisho,
22na Kibzaimu pamoja na maeneo yake ya malisho, na Bethi Horoni pamoja na maeneo yake ya malisho, ilikuwa miji minne kwa ujumla wake.
23Kutoka katika kabila la Dani, ukoo wa Kohathi ulipewa Elteke pamoja na maeneo yake ya malisho, na Gibethoni pamoja na maeneo yake ya malisho, na
24Aijaloni pamoja na maeneo yake ya malisho, na Gathrimoni pamoja na maeneo yake ya malisho, ilikuwa ni miji minne kwa ujumla wake.
25Kutoka katika nusu ya kabila la Manase, ukoo wa Kohathi walipewa miji miwili - Taanaki pamoja na maeneo yake ya malisho na Gathirimoni pamoja na maeneo yake ya malisho.
26Kulikuwa na miji kumi kwa ujumla wake kwa ajili ya koo zilizosalia za Wakohathi, pamoja na maeneo yao ya malisho.
27Kutoka katika nusu ya kabila la Manase, jamaa za Gershoni, ambazo hizi zilikuwa ni koo zingine za Walawi, zilipewa Golani katika Bashani pamoja na maeneo yao ya malisho, ni mji wa makimbilio kwa ajili ya mtu yeyote aliyeua mtu bila kukusudia, sambamba na Beeshitera pamoja na maeneo yake ya malisho - ilikuwa miji miwili kwa ujumla.
28Koo za Gershoni zilipewa pia miji minne kutoka kwa kabila la Isakari - Kishoni sambamba na maeneo yake ya malisho, Daberathi pamoja na maeneo yake ya malisho,
29Yarmuthi pamoja na maeneo yake ya malisho, na Engnimu pamoja na maeneo yake ya malisho.

Read Yoshua 21Yoshua 21
Compare Yoshua 21:8-29Yoshua 21:8-29