Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yoshua - Yoshua 18

Yoshua 18:5-16

Help us?
Click on verse(s) to share them!
5Wataigawanya nchi katika sehemu saba. Yuda itasalia katika eneo lao upande wa kusini, na nyumba ya Yusufu itaendelea katika himaya yao katika upande wa kaskazini.
6Mtaigawanya nchi katika sehemu saba na kisha mtaniletea maelezo hayo hapa kwangu. Nami nitapiga kura kwa ajili yenu hapa mbele za Yahweh Mungu wetu.
7Walawi hana sehemu miongoni mwenu, kwa kuwa ukuhani wa Yahweh ni urithi wao. Makabila ya Gadi, Rubeni na nusu ya kabila la Manase wameshapokea urithi wao ng'ambo ya Yordani. Huu ni urithi ambao Musa mtumishi wa Yahweh aliwapa wao.
8Hivyo, watu waliinuka na wakaenda. Yoshua akawaamuru wale walioenda kuandika maelezo ya nchi, akisema, “Pandeni juu na mshuke chini katika nchi na andikeni maelezo kuhusu nchi na kisha mrejee kwangu. Nitapiga kura kwa ajili yenu hapa mbele za Yahweh huko Shilo.
9Watu walienda na walitembea juu na chini katika nchi na wakaandika maelezo kuihusu nchi hiyo juu ya gombo kwa miji yake katika sehemu saba, kwa kutaja miji, kila mmoja katika sehemu moja. Kisha wakarudi kwa Yoshua katika kambi huko Shilo.
10Kisha Yoshua akapiga kura kwa ajili yao huko Shilo mbele za Yahweh. Na hapo Yoshua akaigawa nchi kwa watu wa Israeli, kila kabila lilipewa sehemu ya nchi.
11Katika kabila la Benyamini, ugawanaji wa nchi ulifanyika kwa kupewa kwa koo zao. Eneo la nchi waliyopewa lilikuwa kati ya wazawa wa Yuda na wazawa wa Yusufu.
12Katika upande wa kusini, mpaka wao ulianzia katika Yordani. Mpaka ulipanda hata sehemu ya juu kaskazini mwa Yeriko, na kisha ukapita katikati ya nchi ya milima upande wa magharibi. Huko ukafika hadi nyika ya Bethi Aveni.
13Kutoka hapo mpaka ulipita upande wa kusini katika mwelekeo wa Luzi (sehemu ile ile inayoitwa Betheli). Kisha mpaka ukashuka chini hata Atarothi Adda, karibu na mlima uliolekea kusini mwa Bethi Horoni.
14Kisha mpaka ukaendelea upande mwingine: katika upande wa magharibi uligeukia upande wa kusini, ulienda mbele kuukabili mlima ulio ng'ambo ya Bethi Horoni. Mpaka huu ulikomea huko Kiriathi Baali (ambao ndio Kiriathi Yearimu), mji ambao ulikuwa ni wa kabila la Yuda. Na huu ndio ulikuwa ni mpaka katika upande wa magharibi.
15Katika upande wa kusini, mpaka ulianzia nje tu ya Kiriathi Yearimu. Mpaka uliendelea kutoka Efroni hata chemichemi ya maji ya Neftoa.
16Kisha mpaka ulishuka chini hadi mpaka wa mlima ambao ulikuwa mkabala ya bonde la Beni Hinomu, ambalo lililokuwa katika upande wa kaskazini mwishoni mwa bonde la Refaimu. Kisha ulishuka chini kuelekea bonde la Hinomu, sehemu ya kusini mwa mteremko wa Wayebusi, na uliendelea kushuka chini hadi Eni Rogeli.

Read Yoshua 18Yoshua 18
Compare Yoshua 18:5-16Yoshua 18:5-16