1Hili ni neno la Yahwe lililomjia Yeremia nabii juu ya mataifa.
2Juu ya Misri; “Hili ni juu ya jeshi la Farao Neko, mfalme wa Misri aliyekuwako Karkemishi kando ya mto Frati. Hili ni jeshi alilolishinda Nebukadneza mfalme wa Babeli likishindwa katika mwaka wa nne wa Yehoyakimu mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda:
3Wekeni tayari ngao ndogo na kubwa, na msonge vitani.
4Watieni farasi lijamu na hatamu, na mpande juu yao, ninyi wapanda farasi. Jiwekeni mahali penu, mkiwa mmevaa helmeti vichwani mwenu. Inoweni mishale yenu na kuvaa silaha zenu.
5Ninaona nini hapa? Wana woga na wanakimbia, maana askari wao wameshindwa. Wanakimbia kwa usalama na hawaangalii nyuma. Kitisho kipo mahali pote - hili ni tamko la Yahwe -
6wepesi hawawezi kukimbia, na askari hawezi kukwepa. Wana jikwaa kaskazini na kuanguaka kando ya mto Frati.
7Ni nani hawa wainukao kama Nile, ambao maji yao yanaruka juu na chini kama mito?
8Misri huinuka kama mto Nile, na maji yake yanaumuka juu na chini kama mito. Anasema, 'nitapanda juu; nitaifunika nchi. Nitaiharibu miji na watu wake.
9Inukeni, farasi. Mwe na hasira, ninyi vibandawazi. Askari na waende, Kushi na Putu, watu walio na ujuzi wa ngao, na Ludimu, watu wenye ujuzi wa kupiga pinde zao.
10Siku hiyo itakuwa siku ya kisasi kwa Bwana Yahwe wa majeshi, naye atajilipizia kisasa juu ya adui zake. Upanga utararua na kujirishisha. Utakula na kujishibisha kwa damu yao. Kwa maana kutakuwa na sadaka kwa Bwana Yahwe wa majeshi katika nchi ya kaskazini kando ya mto Frati.
11Panda Gileadi ujipatie dawa, binti wa Misri uliyebikra. Haifai kwamba unaweka dawa nyingi juu yako. Hakuna uponyaji kwako.
12Mataifa wamesikia kuaibika kwako. Nchi imejawa na maombolezo yako, maana askari anajikwaa juu ya askari; na wote wawili uanguka pamoja.”
13Hili ndilo neno Yahwe alilomwambia nabii Yeremia wakati Nebukadneza mfalme wa Babeli alipokuja na kushambulia nchi ya Misri:
14Toa taarifa kwa Misri na isikiwe katika Migdoli na Memfisi. Wamesema katika Tapenesi, wekeni kituo na mwe imara, kwa maana upanga unakula wote kati yenu.
15Kwa nini Apisi mungu wenu amekimbia? Kwa nini ng'ombe dume mungu wenu hakuweza kusimama? Yahwe amemwangusha chini.
16Ameongeza idadi ya waliojikwaa. Kila askari anaanguka kinyume cha anayefuata. Wanasema, “Inuka. Haya twende nyumbani. Haya na turudi kwa watu wetu, katika nchi yetu ya asili. Na tuuache upanga huu unaotuuwa.”
17Walitangaza pale, “Farao mfalme wa Misri ni kelele tu, ameuacha wasaa wake mbali.”
18Kama niishivyo - hili ni tamko la mfalme - Yahwe wa majeshi kwa jina, kuna mtu atakuja aliye kama Mlima Tabori na Mlima Karmeli kando ya bahari.
19Wekeni masanduku yenu kuyachukua uhamishoni, binti mwishio Misri. Kwani Memfisi haitafaa, magofu. Hakuna atakayeishi huko.
20Misri ni mtamba mzuri sana, lakini mdudu aumaye anakuja kutoka kaskazini. Anakuja.
21Askari wake wakukodiwa ni kama dume la ng'ombe lililonona kati yake. lakini wao pia watageuka na kukimbia. Hawatasimama pamoja, kwani siku yao ya madhara inakuja kunyume chao, wakatik wa kuadhibiwa kwao.
22Misri anatoa sauti kama ya nyoka na kuondoka kwa kutambaa. maana adui yake anajiandaa kinyume chake. Wanamkabili kama mkata miti aliye na shoka.
23Wataangusha misitu - japokuwa ni mingi sana - hili ni tamko la Yahwe. Kwa maana adui watakuwa wengi kuliko nzige, wasiohesabika.
24Binti Misri ataaibishwa. Atawekwa mkononi mwa watu kutoka kaskazini.”
25Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema, “Tazama, niko karibu kumwadhibu Amoni wa Thebesi, Farao, Misri na miungu yake, Farao mfalme wake, na wote wanaomtumaini.
26Nitawaweka katika mkono wa wanaoyaona maisha yao, na katika mkono wa Nebukadneza mfalme wa Babeli na watumishi wake. Kisha baada ya haya Misri itakaliwa kama mwanzo - asema Yahwe.”
27Lakini, wewe Yakobo mtumishi wangu, usihofu. Usifadhaike, Israeli, maana tazama, nitakurudisha kutoka mbali, na uzao wako kutoka nchi ya mateka. Kisha Yakobo atarudi, tafuta amani, na kuwa salama, na hapatakuwa na wa kumwogofya.
28Wewe, mtumishi wangu Yakobo, usiogope - asema Yahwe - kwa maana nipo nawe, hivyo nitaleta maangamizi makamilifu dhidi ya mataifa yote nilikokupeleka. Lakini sitakuharibu kabisa. Hata hivyo nitakuadhibu kwa haki na hakika sitakuacha bila adhabu.”