1Hili ni neno la Yahwe lililokuja kwa Yeremia nabi juu ya Wafilisiti. Neno hili lilimjia kabla Farao hajaishambulia Gaza.
2“Yahwe asema hivi: Tazama, mafuriko ya maji yanainuka huko kaskazini. Yatakuwa kama mto uliofurika! Kisha yataigharikisha nchi na kila kitu ndani yake, miji yake na watu wakaao ndani yake! Kila mtu atapiga kelele ya kuomba msaada, na wakaaji wote wa nchi wataomboleza.
3Kwa sauti ya kukanyaga kwa kwato za farasi wao wenye nguvu, kwa mwungurumo wa vibandawazi vyao na kelele za magurudumu yao, wazazi hawatawasaidia watoto wao kwa sababu ya udhaifu wao.
4Kwa maana siku inakuja itakayowaacha ukiwa Wafilisiti wote, kumwondoa kila mtu aliyesalia anayetaka kuwasaidia. Kwa maana Yahwe anawaangamiza Wafilisiti, waliosalia katika kisiwa cha Kaftori.
5Maombolezo yatakuja juu ya Gaza. Hata kwa Ashikeloni, watu waliosalia bondeni watakuwa kimya. Ni kwa muda gani mtajiondoa katika maombolezo?
6Ole, upanga wa Yahwe! itachukua muda gani hata unyamaze? Rudini alani mwenu! Acha na unyamaze.
7Wawezaje kuwa kimya, maana Yahwe amekuagiza. Amekuamuru kumpiga Ashikeloni na dhidi ya nchi ya pwani ya bahari.