Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yeremia

Yeremia 9

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Kama kichwa changu kingetoa maji, na macho yangu kuwa chemichemi ya machozi! kwa kuwa natamani kulia usiku na mchana kwa ajili yao waliokuwa binti za watu wangu ambao wameuawa.
2Kama mtu anganipatia mahali pa wasafiri nyikani ili nikae, mahali ambapo ningeenda kuwatelekeza watu wangu. Kama ningewaacha, kwa kuwa wote ni wazinzi, kundi la wenye hiana!
3asema BWANA, “Huupinda ulimi wao kana kwamba ni upinde ili wapate kuongea uongo, lakini si kwa uamiinifu wao kwamba wanapata nguvu duniani. Wanatoka uovu mmoja hadi mwiingine. Hawanijui mimi.”
4Kila mmoja wenu, awe mlinzi wa jirani yake na usimwamini hata ndugu yako yeyote. kwa kuwa kila ndugu ni mwongo,
5kila jirani anatembea akilaghai. Kila mwanamume anakejeli jirani yake na haongei ukweli. Ndimi zao hufundisha vitu vya uongo. Hujidhofisha ili kusema uongo.
6Makazi yenu yako kati ya udanganyifu; kwa uongo wao wanakataa kunitambua mimi. Asema BWANA.”
7Kwa hiyo BWANA wa majeshi asema hivi, “Tazama, Niko tayari kuwajaribu. Nitawajaribu nione. Jinsi gani niwezavyo kufanya kwa binti za watu wangu?
8Ndimi zao ni mishale iliyochongoka; huongea vitu vya uasi. Kwa midomo yao wanatangaza amani pamoja na jirani zao, lakini katika mioyo yao wanadanganya wakati wa kusubri.
9Kwa nini nisiwaadhibu kwa sababu ya mambo haya - asema BWANA na kwa nini nisijilipizie kisasi kwa taifa ambalo liko kama hili?
10Nitaimba wimbo wa kuomboleza na kulia kwa ajili ya milima, na wimbo wa mazishi utaimbwa nyikani. Kwa kuwa wameteketezwa kwa hiyo hakuna anAyeweza kupita kati kati yao. Hawatasikia sauti ya ng'ombe yeyote. Ndege wa angani na wanyama wote wamekimbia.
11Kwa hiyo nitaigeuza Yerusalemu kuwa vifusi vya ukiwa, maficho ya mbweha. Nitaifanya miji ya Yuda kuwa miji iliyoharibiwa isiyokaliwa na watu.
12Ni nani mwenye hekima anayeyaelewa haya? Je, kinywa cha BWANA kinatangaza nini kwake ili aweze kuyasema? Kwa nini nchi imepotea? Imeharibiwa kama jangwa, ambapo hakuna apitaye kati kati yake.
13BWANA asema, “Ni kwa sababu wameziacha sheria zake ambazo niliwatengenezea, kwa sababu hawaisikilizi sauti yangu au kuishi kwa kuifuta.
14Ni kwa sababu wameishi kwa ushupavu wa mioyo yao na wamewafuata Mabaali kama baba zao walivyowafundisha kufanya.
15Kwa hiyo BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, 'Tazama, Ninataka kuwafanya hawa watu wale pakanga na kunywa maji ya sumu.
16Ndipo nitakapowasambaza kati ya mataifa ambayo hawajayajua, wao wala mababu zao. Nitatuma upanga kwa ajili yao mpaka nimewaangamiza wote kabisa.'”
17BWANA wa majeshi asema hivi, “Yafikirini haya: Waiteni waliaji; waje. Tumeni wanawake wenye taaluma ya kuomboleza, waje.
18Waje haraka waimbe wimbo wa maombolezo juu yetu, ili macho yetu yatokwe na machozi na kope zetu zibubujikwe na maji.

19Kwa kuwa sauti ya kilio imesikika Sayuni, 'Jinsi tulivyoharibiwa. Tumeaibishwa sana, kwa kuwa tumeitelekeza nchi tangu walIpoangusha nyumba zetu.'
20Kwa hiyo ninyi wanawake, sikieni neno la BWANA; zingatieni ujumbe unaokuja toka kinywani mwake. Kisha wafundisheni binti zenu wimbo wa maombolezo, na kila mwanamke wa jirani wimbo wa kilio.
21Kwa kuwa vifo vimekuja kupitia dirishani; vinaelekea mahali petu. Vinawaharibu watoto kutoka nje na vijana kwenye viwanja vya miji.
22Uyatangaze haya, 'Asema BWANA - mizoga ya wanaume itaanguka kama mavi kwenye mashamba na kama mabua baada ya mvunaji, na hapatakuwa na mtu wa kuyakusanya.'”
23BWANA asema hivi, “Usimwache mtu mwenye busara ajivune kwa ajili ya hekima yake, au shujaa kwa sababu ya uwezo wake. Usimwache mtu tajiri ajivunie utajiri wake.
24Kwa kuwa kama mtu atajivunia chochote kile, acha iwe hivi, yeye awe na busra na kunijua mimi. Kwa kuwa mimi ni BWANA, atendaye katika agano la wema, haki, na hukumu duniani. Ni katika hili kwamba ninafurahia- asema BWANA.
25Tazama, siku zaja - asema BWANA wakati nitakapowaadhibu wote ambao hawajatahiriwa ambao wako hivyo hivyo katika miili yao.
26Nitaiadhibu Misri na Yuda, Edomu, watu wa Amoni, Moabu, na watu wote wanaonyoa denge. Kwani mataifa yote haya hayajatahiriwa, na nyumba yote ya Israeli ina moyo ambao haujatahiriwa.”