Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yeremia

Yeremia 33

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Kisha neno la Yahwe likaja kwa Yeremia mara ya pili, alipokuwa bado amefungwa ndani ya uwanja wa walinzi, likisema,
2Yahwe muumbaji, anasema hivi—Yahwe, aumbaye ili athibitishishe—Yahwe ndilo jina lake,
3'Niite, na nitakuitika, nitakuelezea mambo makuu, siri ambazo huzielewi.'
4Kwa maana Yahwe, Mungu wa Israel, anasema hivi kuhusu nyumba zilizo katika mji huu na nyumba za wafalme wa Yuda zilizobomolewa kwa sababu ya maboma na upanga,
5Wakaldayao wanakuja kupigana na kuzijaza nyumba kwa hizi kwa majeshi ya watu ambao wataua katika hasira yangu na ghadhabu yangu, nitakapouficha mji huu uso wangu kwa sababu ya uovu wao wote.
6Lakini ona, niko karibu kuleta uponyaji na tiba, kwa maana nitawaponya na nitawapa wingi wa, amani na uamainifu.
7Kwa maana nitawarudhisha wafungwa wao wa Yuda na Israeli; nitawajenga tena kama ilivyokuw mwanzo.
8Kisha nitawatakasa uovu wote walioufanya dhidi yangu. Nitasamehe makosa yote waliyonitenda, na na njia zote walizo asi dhidi yangu.
9Kwa maana mji huu kwa ajili yangu utakuwa chombo cha furaha, nyimbo, sifa na heshima kwa mataiafa yote ya dunia ambao watasikia mambo yote mema ninayokwenda kufanya kwa ajili ya huu mji. Kisha wataogopa na kutetemeka kwa sababu ya mambo yote mema na amani nitayoupa mji huu.'
10Yahwe anasema hivi, 'Katika sehemu hii ambayo sasa mnaisema, “Imetengwa, sehemu isiyo na mwanadamu wala mnyama,” katika mji huu wa Yuda, na katika mitaa ya Yerusalemu ambayo imetengwa bila mwanadamu wala mnyama, zitasikika tena
11sauti za furaha na sauti za shangwe, sauti ya bwana arusi na sauti ya bibi arusi, sauti za wale wasemao, wanapoleta shukrani katika nyumba ya Yahwe, “Mshukuruni Yahwe wa majeshi, kwa maana Yahwe ni mwema, na upendo wake usioshindwa wadumu milele!” Kwa maana nitawafanaya tena wafungwa wa nchi kuwa walivyokuwa mwanzo,' asema Yahwe.
12Yahwe wa majeshi asema hivi: Katika sehemu hii ya ukiwa, ambamo sasa hakuna mwanadamu wala mnyama—katika miji yake yote kutakuwepo tena malisho ambapo wachungaji wataweza kupumzisha makundi yao.
13Katika miji hii katika nchi ya vilima, nchi tambarare, na Negevu katika nchi ya Benyamini na kuzunguka Yerusalemu yote, na katika miji ya Yuda, makundi yatapata njia chini ya mkono wa yule anayewahesabu,' asema Yahwe.
14Angalia! Siku zinakuja—hili ni tangazo la Yahwe—ambapo nitafanya niliyoahidi kwa nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda.
15Katika siku hizo na katika wakati huo nitachipua shina la haki kwa ajili ya Daudi, na litafanaya hukumu na haki katika nchi.
16Katika siku hizo Yuda wataokolewa, na Yurusalemu utaishi katika usalama, kwa maana hivi ndivyo atakavyoitwa, “Yahwe ni haki ni haki yetu.”
17Kwa maana Yahwe anasema hivi: 'Mwana kutoka ukoo wa Daudi hatakosa kuketi katika kiti cha nyumba ya Israeli,
18wala mtu kutoka ukuhani wa Kilawi hatakosa kutoa sadaka za kuteketezwa mbele zangu, kutoa sadaka za chakula, na kutoa sadaka za nafaka wakati wote.”'

19Neno la Yahwe likaja kwa Yeremia, likisema,
20“Yahwe anasema hivi: 'Kama mkiweza kulivunja agano langu la mchana na usiku ili kwamba siku isikawie wala usiku usikawie kuja kwa wakati wake,
21basi mtaweza u kulivunja agano langu na Daudi mtumishi wangu, ili kwamba aspate mwana wa kuketi juu ya kiti chake cha enzi, na gano langu na makuhuni wa Kilawi, watumishsi wangu.
22Kama vile majeshsi ya mbinguni yasivyoweza kuhesabika, na kama vile mchanga wa ufukwe wa bahari usivyoweza kupimwa, ndivyo nitakavyouongeza uzao wa Daudi mtumishi wangu na Walawi watumikao mbele zangu.”
23Neno la Mungu likaja kwa Yeremia, likisema,
24Hamkuzingatia walichotangaza watu hawa waliposema, 'Zile Familia mbili ambazo Yahwe alizichagua, sasa amezikataa'? Kwa jinsi hii hii waliwapuuza watu wangu, wakisema kwamba si taifa tena katika macho yao.
25Mimi, Yahwe, nasema hivi, 'Kama sijalithibitisha agano la mchana na usiku, na kama sijaziweka sheria za mbingu na dunia,
26basi nitawakataa uzao wa Yakobo na Daudi mtumishi wangu, na nisilete mtu kutoka kati yao wa kutawala juu ya uzao wa Abrahamu, Isaka, na Yakobo. Kwa maana nitawarudisha wafubgwa wao na kuonesha huruma kwao.”'