Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yeremia

Yeremia 37

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Sasa Sedekia mwana wa Yosia alitawala kama mfalme badala ya Yehoyachin mwana wa Yehoyakimu. Nebukadreza mfalme wa Babeli alikuwa amemfanya Sedekia mfalme juu ya nchi ya Yuda.
2Lakini Sedekia, wajakazi wake, na watu wa nchi hawakusikiliza maneno ya Yahwe ambayo alitangaza kwa mkono wa Yeremia nabii.
3Kwa hiyo Mfalme Sedekia, Yehukali mwana wa Shelemia, na Zefania mwana wa Maaseia kuhani alituma ujumbe kwa Yeremia nabii. Walisema, “Omba kwa niaba kwa Yahwe Mungu wetu.”
4Sasa Yeremia alikuwa anakuja na kwenda miongoni mwa watu, kwa kuwa alikuwa bado hajawekwa ndani ya gereza.
5Jeshi la Farao lilitoka Misri, na Wakaldayo waliozingira Yerusalem walisikia habari kuhusu wao na kuondoka Yerusalem.
6Kisha neno la Yahwe lilikuja kwa Yeremia nabii na kusema,
7“Yahwe, Mungu wa Israel, asema hivi: Hiki ndivyo utakavyosema kwa mfalme wa Yuda, kwa sababu amekutuma wewe kutafuta ushauri toka kwangu, 'Ona, jeshi la Farao, ambalo lilikuja kukusaidia, liko tayari kurudi Misri, kwenye nchi yao.
8Wakaldayo watarudi. Watapigana dhidi ya mji huu, kuuteka, na kuuchoma.'
9Yahwe asema hivi: Msidaganyane kwa kusema, “Hakika Wakaldayo wanatuacha sisi,' kwa kuwa hawatatuacha.
10Hata kama mmelishinda jeshi la Wakaldayo lote ambalo linapigana nanyi ili kwamba wanaume waliojeruhiwa walibakizwa katika mahema yao, wangeweza kunyanyuka na kuchoma mji huu.”
11Basi ilikuwa wakati jeshi la Wakaldayo lilipoondoka Yerusalem wakati jeshi la Farao lilikuwa linakuja,
12kisha Yeremia alienda toka Yerusalem kwenda nchi ya Benjamini. Alitaka kumiliki njia ya nchi huko miongoni mwa watu wake.
13Kama alivyokuwa katika mlango wa Benjamini, mlinzi mkuu aliyekuwa hapo. Jina lake lilikuwa Yeria mwana wa Shelemia mwana wa Hanania. Alimshika kwa kumnyakua Yeremia nabii na kusema, “Mnatoka jangwani kwa Wakaldayo.”
14Lakini Yeremia alisema, “Hiyo si kweli. Siendi jangwani kwa Wakaldayo.” Lakini Yeria hakumsikiliza. Alimchukua Yeremia na kumleta kwa maafisa.
15Maafisa walikuwa wamemkasirikia Yeremia. Walimpiga na kumweka gerezani, ambayo ilikuwa nyumba ya Yonathani mwandishi, kwa kuwa waligeuza kuwa gereza.
16Kwa hiyo Yeremia alikuwa amewekwa kwenye kifungo cha chini, ambako alikuwa huko kwa siku nyingi.
17Kisha mfalme Sedekia alimtuma mtu mmoja aliyemleta kwenye ikulu. Kwenye nyumba yake, mfalme alimuuliza binafsi, “Kuna neno: Utatiwa kwenye mkono wa mfalme wa Babeli.”
18Kisha Yeremia alisema kwa mfalme Sedekia, “Kwa namna gani nimekutenda dhambi, mjakazi wako, au watu hawa kwamba umeniweke mimi kwenye gereza?

19Wako wapi nabii wako, wale waliotabiri kwa ajili yako na kusema mfalme wa Babeli hatakuja dhidi yako au dhidi ya nchi hii?
20Lakini sasa sikiliza, bwana wangu mfalme! Acha ombi langu liwe mbele yako. Usinirudie mimi kwenye nyumba ya Yonathani mwandishi, au nitakufa huko.”
21Kwa hiyo mfalme Sedekia alitoa amri. Wajakazi wake walimwekea mipaka Yeremia katika uwanja wa walinzi. Alipewa mkate kila siku kutoka mtaa wa waokaji mkate, mpaka mkate wote mjini uliisha. Basi Yeremia alibaki kwenye uwanja walinzi.