Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yeremia

Yeremia 21

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Hili ndilo neno lililotoka kwa Bwana kwa Yeremia wakati mfalme Sedekia alimtuma Pashuri mwana wa Malkiya na Sefania mwana wa Maaseya, kuhani. Wakamwambia,
2“Pata ushauri kutoka kwa Bwana kwa ajili yetu, kwa kuwa Nebukadreza, mfalme wa Babeli, analeta vita. Labda Bwana atafanya miujiza kwetu, kama ilivyokuwa zamani, na kumfanya aondoke kwetu.”
3Basi Yeremia akawaambia, “Hivi ndivyo mtakavyomwambia Sedekia
4'Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi: Tazama, niageuza nyuma vyombo vya vita vilivyo mkononi mwenu, ambavyo mnapigana dhidi ya mfalme wa Babeli na Wakaldayo wanaokufunga kutoka nje ya kuta! Kwa maana nitawakusanya katikati ya jiji hili.
5Nami nitapigana nanyi kwa mkono ulioinuka na mkono wenye nguvu, na ukali, ghadhabu, na hasira kubwa.
6Kwa maana nitawaangamiza wenyeji wa mji huu, wanadamu na wanyama, watakufa kwa tauni kali.
7Baada ya hayo- hii ndiyo ahadi ya Bwana-Sedekia mfalme wa Yuda, watumishi wake, watu, na kila mtu aishiye katika mji huu baada ya tauni, upanga na njaa, nitawatia wote mkononi mwa Nebukadreza mfalme wa Babeli, na mikononi mwa adui zao, na katika mkono wa wale wanaotaka uhai wao. Ndipo atawaua kwa makali ya upanga. Hatawahurumia, hatawaokoa, au kuwa na rehema.'
8Basi uwaambie watu hawa, 'Bwana asema hivi Angalia, nitaweka mbele yako njia ya uzima na njia ya mauti.
9Mtu yeyote anayeishi katika mji huu atakufa kwa upanga, njaa, na tauni; lakini mtu yeyote atakayetoka na kuanguka kwa magoti mbele ya Wakaldayo ambao wamefungwa dhidi yako ataishi. Yeye ataokoka na maisha yake.
10Kwa maana nimeweka uso wangu juu ya mji huu ili kuleta maafa na sio kuleta mema-hili ndilo tamko la Bwana. Utatiwa mkononi mwa mfalme wa Babeli naye atauteketeza.'
11Kuhusu nyumba ya mfalme wa Yuda, sikiliza neno la Bwana.
12Nyumba ya Daudi, Bwana asema, “Hukumuni kwa haki asubuhi. Umuokoe yule aliyeibiwa kwa mkono wa mwenye kuonea, au ghadhabu yangu itatoka kama moto na kuchoma, na hakuna mtu anayeweza kuizima, kwa sababu ya matendo yako mabaya.
13Angalia, mwenyeji wa bonde na mwamba wa nchi ya wazi! Mimi niko juu yako, - hii ndiyo ahadi ya Bwana- Mimi ni juu ya mtu yeyote anayesema, 'Ni nani atashuka kutupiga?' au 'Ni nani atakayeingia kwenye nyumba zetu?'
14Nitawaadhibu kutokana na matunda ya matendo yako-hili ndilo tamko la Bwana- na nitawasha moto katika misitu, na utateketeza kila kitu.'”