1“Kama utarudi, Israeli- asema BWANA - ikawa kwangu kwamba umerudi. Kama utaondoa hayo mambo yachukizayo mbele yangu na ukaacha kunikimbia mimi tena,
2na ukaapa hivi, 'kama BWANA aishivyo katika kweli, na haki, na katika hukumu.' mataifa yataniomba baraka, na yatanisifu mimi.
3Kwa kuwa BWANA asema hivi kwa kila mmoja katika Yuda na Yerusalemu; 'Limeni shamba zenu na msipande katika miiba.
4Mtahiriwe kwa BWANA na kuondoa govi za mioyo yenu, ninyi wanaume wa Yuda na wakazi wa Yerusalemu, vinginevyo hasira yangu itawaka kama moto na kuteketeteza, na hakutakuwa na mtu wa kuizima. Hii itatokea kwa sababu ya uovu wa matendo yenu.
5Waambie Yuda na Yerusalemu isikie. Waambie, “pigeni baragumu katika nchi.” Tangazeni, “Kusanyeni pamoja. Twendeni kwenye miji ya Maboma.”
6Inueni ishara za bendera na zielekezeni Sayuni, na kimbilieni usalama! Msibaki, kwa kuwa ninaleta majanga kutokea kaskazini na anguko kubwa.
7Simba anakuja kutokea kwenye kichaka chake na yeye atakayeyaharaibu mataifa ameanza kuja. Anaondoka kwenye eneo lake ili aache hofu katika nchi yenu, kuibadili miji yenu kuwa uharibifu, ambapo hakuna hata mmoja atakayeishi. Kwa sababu hii vaeni magunia, lieni na kuomboleza.
8Kwa kuwa nguvu ya hasira ya BWANA haijaondoka kwetu.
9Ndipo itakapotokea katika siku hiyo - asema BWANA - mioyo ya mfalme na wakuu itakufa. Makuhani watasitaajabu na manabii watashangaa.'”
10Kwa hiyo nikasema, “Ahaa! BWANA. Kwa hakika umewadanganya watu hawa na Yerusalemu kwa kuwaambia, 'Kutakuwa na amani kwenu.' Wakati upanga unawaangukia dhidi ya maisha yao.”
11Wakati huo itasemwa juu ya mji huu na Yerusalemu kuwa, “Upepo uwakao kutoka katika nyanda za jangwani utachukua njia yake kuelekea kwa binti ya watu wangu. Hautapepetwa wala kuwatakasa.
12Upepo ulio na nguvu sana utakaokuja kwa amri yangu, na sasa nitapitisha hukumu dhidi yao.
13Tazama anavamia kama wingu, na magari yake ni kama dhoruba. Farasi wake wana mbio kuliko tai. Ole wetu kwa kuwa tutaharibiwa!
14Itakaseni mioyo yenu kutoka uovu wenu, Yerusalemu, ili kwamba muokolewe. Mawazo yako mabaya yatafikiri juu ya kutenda dhambi mpaka lini?
15Kwa kuwa kuna sauti iletayo habari kutoka Dani, na janga lijalo linasikika kutoka vilele vya milima ya Efraimu.
16Yafanyeni mataifa kulifikiria hili: Tazama, na uwatangazie Yerusalemu kuwa wale watekaji wanakuja kutoka katika nchi ya mbali ili kupiga kelel za vita juu ya miji ya Yuda.
17Watakuwa kama walinzi wa shamba liliolimwa dhidi yake pande zote, kwa kuwa amekuwa mpinzani wangu - asema BWANA -
18tabia na matendo yako yamesababisha haya yatokee kwako. Hii itakuwa adhabu yako. Jinsi itakavyokuwa vibaya kwako! itakupiga moyo wako.
19Moyo wangu! Moyo wangu! Niko katika maumivu ya moyo. Moyo wangu umefadhaika ndani yangu. Siwezi kunyamaza kwa kuwa nasikia sauti za pembe, sauti za vita.
20Anguko baada ya anguko limetangazwa, kwa nchi yote imeharibika mara. Wanaharibu masikani yangu na hema yangu ghafula.
21Vita hivi vitaendelea mpaka lini? Ni mpaka lini nitasikiliza sauti za pembe?
22Kwa kuwa upumbavu wa watu wangu - hawanijui mimi. Ni watu wajinga wasio na ufahamu. Wanaufahamu wa mambo maovu, tena hawajui kutenda mema.
23Niliiona nchi, na kuiona! ilikuwa ukiwa na utupu. Kwa kuwa hapakuwa na taa za mbinguni.
24Nilitazama katka miliima. Tazama, ilikuwa inatetemeka, na vilima vyote vilikuwa vinatikisika.
25Nilitazama. Tazama, hapakuwa na mtu, na ndege wote wa angani walikuwa wamekimbia.
26Nikaangalia. Tazama, mashamba yalikuwa jangwa na miji imeangushwa mbele za BWANA, mbele ya hasira yake.”
27Hiki ndicho BWANA asemacho, “Nchi yote itakuwa uharibifu, lakini sitawaharibu wote kabisa.
28Kwa sababu hii nchi itaomboleza, na mbingu juu zitatiwa giza. Kwa kuwa nimesema haya na kuyakusudia; sitarudi nyuma; Sitaacha kuyatekeleza.
29Kila mji utakimbia kutoka katka kelele za wapandafarasi na wenye pinde; Watakimbilia msituni, Kila mji utapanda hadi mahali pa miamba. Miji itatelekezwa, kwa kuwa hakutakuwa na mtu wa kuishi katika miji hiyo.
30Sasa umeharibiwa, utafanya nini? Japokuwa unavaa mavazi mekundu, unajipamba na mapambo ya dhahabu, na kuyafanya macho yako yaonekane makubwa na kupakwa wanja, wale wanaume waliokutamani sasa wanakukataa. Badala yake wanajaribu kukuua.
31Kwa hiyo nasikia sauti ya maumivu, yenye utungu kama ya mwanamke azaaye mtoto wake wa kwanza, sauti ya binti wa Sayuni. Atwetaye kupata pumzi. Ananyosha mikono yake na kusema, 'Ole wangu mimi! ninazimia kwa sababu ya wauaji hawa.'”