Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 1Samweli

1Samweli 16

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1BWANA akamwambia Samweli, “Utamlilia Sauli kwa muda gani, ikiwa nimemkataa asiwe mfalme juu ya Israeli? Ijaze pembe yako mafuta na uende. Nitakutuma kwa Yese akaaye Bethlehemu, maana nimejichagulia mfalme katika wanawe.
2Samweli akasema, “Jinsi gani nitaenda? Kama Sauli akisikia jambo hili, ataniua.” BWANA akasema, “chukua mtamba na useme, 'Nimekuja kutoa dhabihu kwa BWANA.'
3Umwite Yese aje kwenye dhabihu, nami nitakuonesha kile utakachofanya. Utamtia mafuta kwa ajili yangu yule nitakaye kuambia.”
4Samweli akafanya kama BWANA alivyosema na akaenda Bethlehemu. Wazee wa mji walikuwa wakitetemeka walipokuja kuonana naye na wakasema, “Je, umekuja kwa amani?”
5Naye akasema, “kwa amani; Nimekuja kutoa dhabihu kwa BWANA. Jitoeni wenyewe kwa BWANA kwa ajili ya dhabihu na muandamane nami,” Na akamweka wakfu Yese na watoto wake kwa BWANA, na baadaye aliwaita wote kwenye dhabihu.
6Walipofika, akamwangalia Eliabu na akajisemea mwenyewe kwamba mtiwa mafuta wa BWANA hakika amesimama mbele yake.
7Lakini BWANA akamwambia Samweli, “Usimwangalie sura yake ya nje, au kimo cha umbo lake; kwa sababu nimemkataa. Maana BWANA haangalii kama mtu aangaliavyo; mtu hutazama sura ya nje, bali BWANA huutazama moyo.”
8Kisha Yese akamwita Abinadabu akamwambia apite mbele ya Samweli. Na Samweli akasema, “Hata huyu BWANA hakumchagua.”
9Kisha Yese akmwambia Shama apite karibu. Na Samweli akasema, “Hata huyu BWANA hakumchagua.”
10Yese akawaleta watoto wake saba wakapita mbele ya Samweli. Na Samweli akamwambia Yese, “Hakuna hata mmoja aliyechaguliwa na BWANA kati ya hawa.”
11Kisha Samweli akamuulia Yese, “Je, watoto wako wote wako hapa?” Naye akajibu, “Yupo mdogo kabisa lakini anachunga kondoo.” Samweli akamwambia Yese, “Tuma watu wakamwite; maana hatutakaa chini hadi atakapofika hapa.”
12Yese akawatuma watu wakamleta. Naye kijana huyu alikuwa mwekundu na mwenye macho mazuri na mwenye muonekano mzuri. BWANA akasema, “Amka, umtie mafuta; maana huyu ndiye.”
13Ndipo Samweli akachukua pembe yenye mafuta na kumtia mafuta katikati ya kaka zake. Roho wa BWANA akamwijia Daudi kwa nguvu tangu siku hiyo na kuendelea. Kisha Samweli akanyanyuka na kwenda Rama.
14Basi Roho wa BWANA akamwacha Sauli, badala yake roho ya ubaya kutoka kwa BWANA ikamsumbua.
15Watumishi wa Sauli wakamwambia, “Tazama, roho ya ubaya kutoka kwa Mungu inakusumbua.
16Haya bwana wetu hebu sasa amuru watumishi wako walio mbele yako wamtafute mtu mwenye ujuzi wa kupiga kinubi. Basi ikwa roho wa ubaya kutoka kwa Mungu yuko juu yako, atakipiga kinubi nawe utajisikia vizuri.”
17Sauli akawaambia watumishi wake, “Mnitafutie mtu anayeweza kupiga vizuri na mmlete kwangu.”
18Ndipo kijana mmoja kati yao akajibu, na kusema, “Nimemuona mtoto wa Yese Mbethtelehemu, aliye mjuzi katika kupiga, ni mwenye nguvu, mtu jasiri, mtu wa vita, mwenye busara aongeapo, mtu mzuri kwa uso; na BWANA yuko pamoja naye.”

19Hivyo Sauli akawatuma wajumbe kwa Yese, na kusema, “Nitumie mtoto wako Daudi, anayewatunza kondoo.” 1 Samweli! 6: 20-21
20Yese akamchukua punda aliyebeba mikate, na kiriba cha divai, na mwana-mbuzi, na akamtuma kwa Sauli pamoja na vitu hivyo.
21Ndipo Daudi akafika kwa Sauli na kuanza kazi yake. Sauli alimpenda sana Daudi, na akawa mbeba silaha wake.
22Sauli akawatuma wajumbe kwa Yese, akisema, “Mruhusu Daudi awe mbele yangu, maana amepata kibali machoni pangu.”
23Wakati wowote roho ya usumbufu kutoka kwa Mungu ikiwapo juu ya Sauli, Daudi alichukuwa kinubi na kukipiga. Hivyo Sauli angeburudishwa na kupona, na huyo roho wa usumbufu angemtoka.