Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Luka - Luka 5

Luka 5:1-13

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Basi ilitokea wakati watu walipomkusanyikia na kumzunguka Yesu na kusikiliza neno la Mungu, ambapo alikuwa amesimama kando ya ziwa Genesareti.
2Aliona mashua mbili zimetia nanga pembeni mwa ziwa. Wavuvi walikuwa wametoka na walikuwa wakiosha nyavu zao.
3Yesu akaingia katika mojawapo ya zile mashua, ambayo ilikuwa ya Simoni na kumwomba aipeleke majini mbali kidogo na nchi kavu. Kisha akakaa na kufundisha kutokea kwenye mashua.
4kuongea, akamwambia Simoni, “Ipeleke mashua yako mpaka kwenye kilindi cha maji nakushusha nyavu zako ili kuvua samaki.”
5Simon akajibu na kusema, Bwana, tumefanya kazi usiku wote, na hatukukamata chochote, lakini kwa neno lako, nitazishusha nyavu.
6Walipofanya hivyo walikusanya kiasi kikubwa cha samaki na nyavu zao zikaanza kukatika.
7Hivyo wakawaashiria washirika wao kwenye mashua nyingine ili waja na kuwasaidia. Walikuja wakazijaza mashua zote, kiasi kwamba zikaanza kuzama.
8Lakini Simoni Petro, alipoona hivyo, alianguka magotini pa Yesu akisema, “Ondoka kwangu, kwa sababu mimi ni mtu mwenye dhambi Bwana.”
9Kwa sababu alishangazwa, na wote waliokuwa pamoja naye, kwa uvuvi wa samaki waliokuwa wameufanya.
10Hili liliwajumuisha Yakobo na Yohana wana wa Zebedayo, ambao walikuwa washirika wa Simoni. Na Yesu akamwambia Simoni, “Usiogope, kwa sababu kuanzia sasa na kuendelea utavua watu.”
11Walipokwishazileta mashua zao nchi kavu, waliacha kila kitu na kumfuata yeye.
12Ilitokea kwamba alipokuwa katika mji mmojawapo, mtu aliyekuwa amejaa ukoma alikuwa huko. Wakati alipomuona Yesu, alianguka akiinamisha uso kwake mpaka chini na kumuomba, akisema, “Bwana, ikiwa unataka, waweza kunitakasa.”
13Kisha Yesu alinyoosha mkono wake na kumgusa, akisema, “Nataka. Takasika.” Na saa ileile ukoma ukamwacha.

Read Luka 5Luka 5
Compare Luka 5:1-13Luka 5:1-13