Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Luka - Luka 1

Luka 1:54-65

Help us?
Click on verse(s) to share them!
54Ametoa msaada kwa Israeli mtumishi wake, ili kukumbuka kuonesha rehema
55(kama alivyosema kwa baba zetu) kwa Abrahamu na uzao wake milele.”
56Mariamu alikaa na Elizabeti yapata miezi mitatu hivi ndipo akarudi nyumbani kwake.
57Sasa wakati ulikuwa umewadia kwa Elizabeti kujifungua mtoto wake na akajifungua mtoto wa kiume.
58Jirani zake na ndugu zake walisikia jinsi Bwana alivyoikuza rehema kwake, na wakafurahi pamoja naye.
59Sasa ilitokea siku ya nane kwamnba walikuja kumtahiri mtoto. Ingewapasa kumwita jina lake, “Zekaria,” kwa kuzingatia jina la baba yake,
60Lakini mama yake akajibu na kusema, “Hapana; ataitwa Yohana.”
61Wakamwambia, hakuna hata mmoja katika ndugu zako anayeitwa kwa jina hili.”
62Wakamfanyia ishara baba yake kuashiria yeye alitaka jina aitwe nani.
63Baba yake akahitaji kibao cha kuandikia, na akaandika, “Jina lake ni Yohana.” Wote wakashangazwa na hili.
64Ghafla mdomo wake ukafunguliwa na ulimi wake ukawa huru. Akaongea na kumsifu Mungu.
65Hofu ikawajia wote walioishi karibu nao. Mambo haya yakaenea katika nchi yote ya vilima vya Yudea.

Read Luka 1Luka 1
Compare Luka 1:54-65Luka 1:54-65