Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Luka 1:54-65 in Swahili (individual language)

Help us?

Luka 1:54-65 in Biblia Takatifu

54 Amemsaidia Israeli mtumishi wake, akikumbuka huruma yake.
55 Kama alivyowaahidia wazee wetu Abrahamu na wazawa wake hata milele.”
56 Maria alikaa na Elisabeti kwa muda upatao miezi mitatu, halafu akarudi nyumbani kwake.
57 Wakati wa kujifungua kwake Elisabeti ulifika, akajifungua mtoto wa kiume.
58 Jirani na watu wa jamaa yake walipopata habari kwamba Bwana amemwonea huruma kubwa, walifurahi pamoja naye.
59 Halafu siku ya nane walifika kumtahiri mtoto, wakataka kumpa jina la baba yake, Zakariya.
60 Lakini mama yake akasema, “La, sivyo, bali ataitwa Yohane.”
61 Wakamwambia, “Mbona hakuna yeyote katika ukoo wake mwenye jina hilo?”
62 Basi, wakamwashiria baba yake wapate kujua alitaka mtoto wake apewe jina gani.
63 Naye akaomba kibao cha kuandikia, akaandika hivi: “Yohane ndilo jina lake.” Wote wakastaajabu.
64 Papo hapo midomo na ulimi wake Zakariya vikafunguliwa, akawa anaongea akimsifu Mungu.
65 Hofu ikawaingia jirani wote, na habari hizo zikaenea kila mahali katika milima ya Yudea.
Luka 1 in Biblia Takatifu

Luka 1:54-65 in Biblia ya Kiswahili

54 Ametoa msaada kwa Israeli mtumishi wake, ili kukumbuka kuonesha rehema
55 (kama alivyosema kwa baba zetu) kwa Abrahamu na uzao wake milele.”
56 Mariamu alikaa na Elizabeti yapata miezi mitatu hivi ndipo akarudi nyumbani kwake.
57 Sasa wakati ulikuwa umewadia kwa Elizabeti kujifungua mtoto wake na akajifungua mtoto wa kiume.
58 Jirani zake na ndugu zake walisikia jinsi Bwana alivyoikuza rehema kwake, na wakafurahi pamoja naye.
59 Sasa ilitokea siku ya nane kwamnba walikuja kumtahiri mtoto. Ingewapasa kumwita jina lake, “Zekaria,” kwa kuzingatia jina la baba yake,
60 Lakini mama yake akajibu na kusema, “Hapana; ataitwa Yohana.”
61 Wakamwambia, hakuna hata mmoja katika ndugu zako anayeitwa kwa jina hili.”
62 Wakamfanyia ishara baba yake kuashiria yeye alitaka jina aitwe nani.
63 Baba yake akahitaji kibao cha kuandikia, na akaandika, “Jina lake ni Yohana.” Wote wakashangazwa na hili.
64 Ghafla mdomo wake ukafunguliwa na ulimi wake ukawa huru. Akaongea na kumsifu Mungu.
65 Hofu ikawajia wote walioishi karibu nao. Mambo haya yakaenea katika nchi yote ya vilima vya Yudea.
Luka 1 in Biblia ya Kiswahili