Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Hesabu - Hesabu 19

Hesabu 19:2-6

Help us?
Click on verse(s) to share them!
2“Hii ni amri, ni sheria ninayokuamuru: Waambie wana waIsraeli wakuletee ng'ombe mke mwekundu asiyekuwa na kipaku wala waa, ambaye hajawahi kubeba nira.
3Mpatie Eliazari kuhani huyo ng'ombe jike. Naye atamtoa nje ya kambi, na mtu mmoja amchinje mbele yake.
4Kisha Eliazari kuhani atachukua sehemu ya damu yake kwa kidole chake na kuinyunyiza mara saba akielekea sehemu ya mbele ya ile hema ya kukutania.
5Na kuhani mwingine atamchoma huyo ng'ombe mbele ya macho yake. Ataichoma ngozi yake, nyama yake, na damu yake pamoja na mavi yake,
6Yule kuhani atachukua mti wa mwerezi, na hisopo na sufu na kivitupa katikati ya huyo ng'ombe anayechomwa.

Read Hesabu 19Hesabu 19
Compare Hesabu 19:2-6Hesabu 19:2-6