1Modeka aliposikia kilichokuwa kimepangwa dhidi yao, alirarua mavazi yake na kuvaa maguni na majivu. Akaenda katikati mwa mji na kulia kwa sauti na uchungu mwingi.
2Akaenda hadi langoni mwa mfalme; kwa sababu hakuna aliye ruhusiwa kuingia akiwa amevaa magunia.
3Amri hii ilipofika katika kila jimbo, kulikuwa na kilio kikubwa kwa Wayahudi, na kufunga, kulia na maombolezo. Wengi wao walilala katika magunia na majivu.
4Malkia Esta alipopata habari kutoka kwa wahudumu wake, alipatwa na majonzi. Akatuma watu wampelekee nguo Modekai ili avue magunia na kuvaa nguo nzuri, lakini Modekai hakukubali.
5kisha Esta akamwita Hathaki, mmoja wa wasimamizi wa mfalme, ambaye alikuwa amepewa wajibu wa kumuhudumia. Akamwagiza kwenda kwa Modekai ili afahamu kwa nini Modekai ameamua kufanya hivyo.
6Hivyo Hathaki akaenda kwa Modekai katika mji mbele ya lango la mfalme.
7Modekai akamweleza Hathaki mambo yote kuhusu maangamizi ya Wayahudi yaliyo pangwa na kiasi cha fedha ambacho Hamani ameahidi kuwapa wahazini wa mfalme, ili kuwaua Wayahudi.
8Na kisha akampa nakala ya mbiu ambayo ilitolewa Shushani kwa uangamivu wa Wayahudi. Alifanya hiivyo ili kwamba Hathaki amwambie Esta achukue jukumu la kwenda na kumuomba mfalme na kumsihi kwa niaba ya Wayahudi.
9Hivyo, Hathaki akaenda na kumweleza Esta kile alicho ambiwa na Modekai.
10Esta akaongea na Hathaki na akamwambia arudi kwa Modekai.
11Esta akamwambia Hathaki, “Watumishi wote wa mfalme na watu wote katika majimbo yote wanafahamu kuwa mtu yeyote aingiae kwa mfalme bila kibali anapaswa kufa isipokuwa yule ambaye mfalme atamunyoshea fimbo yake ya dhahabu. Ni siku thelathini sasa sijaenda mbele ya mfalme.
12Hathaki akamwambia Modekai maneno aliyoambiwa na Esta.
13Modekai akarudisha ujumbe: “usifikiri kwamba wewe utasalimika kuliko Wayahudi wote.
14Kama ukikaa kimya kwa wakati huu, Mungu ataleta wokovu kwa njia nyingine, lakini wewe na nyumba ya baba yako mtaangamia. Ni nani ajuaye umekuja katika nafasi hii kwa wakati muafaka kama huu.
15Kisha Esta akatuma ujumbe kwa Modekai,
16“Nenda, uwakusanyea Wayahudi wote wanaoishi katika mji wa Shushani, na wafunge kwa ajili yangu. Wasile wala kunywa kwa muda wa siku tatu. Mimi na watumishi watumishi wangu wa kike tutafunga kwa siku hizo. Na kisha nitaenda mbele ya mfalme kinyume cha sheria. Na kama nitakufa na nife.
17Modekai akaenda na akafanya yote ambayo Esta aliyo mwagiza kufanya.