Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Esta

Esta 7

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Kwa hiyo mfalme na Hamani wakaenda kausherekea na malkia Esta.
2Katika siku ya pili, baada ya kuletwa mvinyo, mfalme akamwambia Esta, “Ni nini haja ya moyo wako? Na nini ombi lako? Hata nusu ya ufalme wangu utapewa.”
3Kisha Malkia amwambia mfalme, kama nimepata kibali machoni pako, na kama ikikupendeza, nipewe maisha yangu, na hili ndio haja ya moyo wangu, na hili pia ni ombi kwa watu wangu pia.
4Kwa kuwa mimi na watu wangu tumeuzwa, ili tuharibiwe, tuuwawe, na tungamizwe. Kama tungeuzwa utumwani, kama wanaume na wanawake, ningenyamaza kimya, na nisingeweza kumsumbua mfame.”
5Kisha Mfalme Ahusiero akamwambia malkia Esta, “Ni nani huyo? Ni nani aliyekusudia moyoni mwake kutenda jambo hili?
6Esta akasema, “Ni huyu mwovu Hamani, adui!” Hamani akashikwa na Hofu mbele za mfalme na malkia.
7Na kwa ghadhabu mfalme akatoka karamuni katika sehemu ya mvinyo na akaenda katika bustani ya ikulu, Lakini Hamani alibaki akimsihi Malkia Esta ili aokoe maisha yake. Kwa sababu aliona mfalme amemkusudia ubaya.
8Mfalme akarudi kutoka katika bustani ya ikulu, na kuingia katika chumba ambamo kulikuwamo mvinyo. Hamani alikuwa ameanguka chini ya kochi alilokuwa ameketi Esta. Mfalme akakasirika na kusema, “atamdharirisha malkia mbele zangu katika nyumba yangu?” Mara tu maneno haya yalipotoka kinywani mwa mfalme, watumizhi wakafunika uso wa Hamani.
9Kisha Habona, mmoja wa watumishi aliye mtumikia mfalme akamwambia mfalme, “Mti wenye urefu wa futi hamsini uko nyumbani kwa Hamani. Ulikuwa umeandaliwa kwa ajili ya Modekai, aliye toa taarifa kuhusu mpango wa kuangamizwa kwako.” Mfalme akesema, “Mtundikeni Hamani juu yake.”
10Kwa hiyo wakamtundika Hamani kwenye mti aliuandaa kwa ajili ya Modekai. Na hasira ya mfalme ikatulia.