Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Wafilipi - Wafilipi 4

Wafilipi 4:10-14

Help us?
Click on verse(s) to share them!
10Ninayo furaha kubwa sana juu yenu katika Bwana kwa kuwa ninyi mmeonyesha tena nia ya kujihusisha kwenu juu ya mahitaji yangu. Kwa kweli, hapo awali mlitamani kunijali kwa mahitaji yangu japo hamkupata fursa ya kunisaidia.
11Sisemi hivyo ili kujipatia kitu kwa ajili ya mahitaji yangu. Kwani nimejifunza kuridhika katika hali zote.
12Nafahamu kuishi katika hali ya kupungukiwa na pia katika hali ya kuwa na vingi. Katika mazingira yote haya mimi nimejifunza siri ya namna ya kula wakati wa shibe na jinsi ya kula wakati wa njaa, yaani vingi na kuwa mhihtaji.
13Ninaweza kufanya haya kwa kuwezeshwa na Yeye anitiaye nguvu.
14Hata hivyo, mlifanya vyema kushiriki nami katika dhiki zangu.

Read Wafilipi 4Wafilipi 4
Compare Wafilipi 4:10-14Wafilipi 4:10-14