Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 2 Wakorintho

2 Wakorintho 12

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Ni lazima nijivune, lakini hakuna kinachoongezwa na hilo. Bali nitaendelea kwenye maono na mafunuo kutoka kwa Bwana.
2Namjua mtu mmoja katika Kristo ambaye miaka kumi na minne iliyopita ambaye—ikiwa katika mwili, au nje ya mwili, mimi sijui, Mungu anajua—alinyakuliwa juu katika mbingu ya tatu.
3Na ninajua kwamba mtu huyu—ikiwa katika mwili, au nje ya mwili, mimi sijui, Mungu anajua—
4alichukuliwa juu hadi paradiso na kusikia mambo matakatifu sana kwa mtu yeyote kuyasema.
5Kwa niaba ya mtu kama huyo nitajivuna. lakini kwa niaba yangu mwenyewe sitajivuna. Isipokuwa kuhusu udhaifu wangu.
6Kama nikitaka kujivuna, nisingekuwa mpumbavu, kwa kuwa ningekuwa ninazungumza ukweli. Lakini nitaacha kujivuna, ili kwamba asiwepo yeyote atakayenifikiria zaidi ya hayo kuliko kinachoonekana ndani yangu au kusikika kutoka kwangu.
7Sitajivuna pia kwa sababu ya hayo mafunuo ya aina ya ajabu. Kwa hiyo, hivyo sitajawa na kiburi, mwiba uliwekwa ndani ya mwili wangu, mjumbe wa shetani kunishambulia mimi, ili nisigeuke kuwa mwenye majivuno.
8Mara tatu nilimsihi Bwana kuhusu hili, ili yeye kuundoa kutoka kwangu.
9Naye akaniambia, “Neema yangu inatosha kwa ajili yako, kwa kuwa nguvu hufanywa kamili katika udhaifu. Hivyo, ningetamani zaidi kujivuna zaidi kuhusu udhaifu wangu, ili kwamba uwezo wa Kristo uweze kukaa juu yangu.
10Kwa hiyo ninatosheka kwa ajili ya Kristo, katika udhaifu, katika matukano, katika shida, katika mateso, katika hali ya masikitiko. Kwa kuwa wakati nikiwa dhaifu, kisha nina nguvu.
11Mimi nimekuwa mpumbavu! ninyi mlinilazimisha kwa hili, kwa kuwa ningekuwa nimesifiwa na ninyi. Kwa kuwa sikuwa duni kabisa kwa hao waitwao mitume—bora, hata kama mimi si kitu.
12Ishara za kweli za mtume zilifanyika katikati yenu kwa uvumilivu, ishara na maajabu na matendo makuu.
13Kwa namna gani mlikuwa wa muhimu wa chini kuliko makanisa yaliyobaki, isipokuwa kwamba sikuwa mzigo kwenu? Mnisamehe kwa kosa hili!
14Tazama! mimi niko tayari kuja kwenu kwa mara ya tatu. Sitakuwa mzigo kwenu, kwa kuwa sitaki kitu kilicho chenu. Nawataka ninyi. Kwa kuwa watoto hawapaswi kuweka akiba kwa ajili ya wazazi. Badala yake, wazazi wanapaswa kuweka akiba kwa ajili ya watoto.
15Nitafurahi zaidi kutumia na kutumiwa kwa ajili ya nafsi zenu. Kama ninawapenda zaidi, natakiwa kupendwa kidogo?
16Lakini kama ilivyo, sikuwalemea mzigo ninyi. Lakini kwa kuwa mimi ni mwerevu sana, mimi ni yule aliyewashika ninyi kwa nimekuwa ambaye aliyewapata kwa udanganyifu.
17Je, nilichukua kwa kujifanyia faida kwa yeyote niliyemtuma kwenu?
18Nilimsihi Tito kuja kwenu, na nilituma ndugu mwingine pamoja naye. Je, Tito aliwafanyia faida ninyi? Je, hatukutembea katika njia ile ile? Je, hatukutembea katika nyayo zile zile?

19Mnadhani kwa muda huu wote tumekuwa tukijitetea sisi wenyewe kwenu? Mbele za Mungu, na katika Kristo, tumekuwa tukisema kila kitu kwa ajili ya kuwaimarisha ninyi.
20Kwa kuwa nina hofu kwamba nitakapokuja naweza nisiwapate ninyi kama ninavyotamani. Nina hofu kwamba mnaweza msinipate mimi kama mnavyotamani. Nahofia kwamba kunaweza kuwa na majadiliano, wivu, milipuko ya hasira, tamaa ya ubinafsi, umbeya, kiburi, na ugomvi.
21Nina hofu kwamba nitakaporudi tena, Mungu wangu anaweza kuninyenyekeza mbele yenu. Nina hofu kwamba ninaweza kuhuzunishwa na wengi ambao wamefanya dhambi kabla ya sasa, na ambao hawakutubu uchafu, na uasherati na mambo ya tamaa wanayoyatenda.