Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 2 Wakorintho

2 Wakorintho 9

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Kuhusiana na huduma kwa ajili ya waumini, ni bora zaidi kwangu kuwaandikia.
2Ninajua kuhusu shauku yenu, ambayo nilijivunia kwa watu wa Makedonia. Niliwaambia kwamba Akaya imekuwa tayari tangu mwaka uliopita. Hamu yenu imewatia moyo wengi wao kutenda.
3Sasa, nimewatuma ndugu ili kwamba majivuno yetu kuhusu ninyi yasiwe ya bure, na ili kwamba mngekuwa tayari, kama nilivyosema mngekuwa.
4Vinginevyo, kama mtu yeyote wa Makedonia akija pamoja nami na kuwakuta hamjawa tayari, tungeona haya — sisemi chochote kuhusu ninyi—kwa kuwa jasiri sana katika ninyi.
5Hivyo niliona ilikuwa muhimu kuwasihi ndugu kuja kwenu na kufanya mipango mapema kwa ajili ya zawadi mlizoahidi. Hii ni hivyo ili kwamba ziwe tayari kama baraka, na si kama kitu kilichoamriwa.
6Wazo ni hili: mtu apandaye haba pia atavuna haba, na yeyote apandaye kwa lengo la baraka pia atavuna baraka.
7Basi na kila mmoja atoe kama alivyopanga moyoni mwake. Basi naye asitoe kwa huzuni au kwa kulazimishwa. Kwa kuwa Mungu humpenda yule atoaye kwa furaha.
8Na Mungu anaweza kuizidishia kila baraka kwa ajili yenu, ili kwamba, kila wakati, katika mambo yote, muweze kupata yote mnayohitaji. Hii itakuwa ili kwamba mueze kuzidisha kila tendo jema.
9Ni kama ilivyoandikwa: “Ametapanya utajiri wake na kuutoa kwa maskini. Haki yake yadumu milele.”
10Naye atoaye mbegu kwa mpanzi na mkate kwa ajili ya chakula, pia atatoa na kuzidisha mbegu yenu kwa ajili ya kupanda. Yeye ataongeza mavuno ya haki yenu.
11Mtatajirishwa kwa kila namna ili kwamba muweze kuwa wakarimu. Hii italeta shukrani kwa Mungu kupitia sisi.
12Kwa kufanya huduma hii sio tu inagusa mahitaji ya waumini. Pia huzidisha katika matendo mengi ya shukrani kwa Mungu.
13Kwa sababu ya kupimwa kwenu na kuthibitishwa kwa huduma hii, pia mtamtukuza Mungu kwa utii kwa ukiri wenu wa injili ya Kristo. Pia mtamtukuza Mungu kwa ukarimu wa karama yenu kwao na kwa kila mmoja.
14Wanawatamani, na wanaomba kwa ajili yenu. Wanafanya hivi kwa sababu ya neema kubwa ya Mungu iliyo juu yenu.
15Shukrani ziwe kwa Mungu kwa karama yake isiyoelezeka!