Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 2 Wakorintho

2 Wakorintho 3

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Je, tumeanza kujisifia wenyewe tena? Hatuhitaji barua ya mapendekezo kwenu au kutoka kwenu, kama baadhi ya watu, je twahitaji?
2Ninyi wenyewe ni barua yetu ya mapendekezo, iliyoandikwa kwenye mioyo yetu, inayojulikana na kusomwa na watu wote.
3Na mnaonesha kwamba ninyi ni barua kutoka kwa Kristo, iliyotolewa na sisi. Iliandikwa siyo kwa wino bali kwa Roho wa Mungu aliye hai. Haikuandikwa juu ya vibao vya mawe, bali juu ya vibao vya mioyo ya wanadamu.
4Na huu ndiyo ujasiri tulio nao katika Mungu kupitia Kristo.
5Hatujiamini wenyewe kwa kudai chochote kama kutoka kwetu. Badala yake, kujiamini kwetu kunatoka kwa Mungu.
6Ni Mungu ambaye alitufanya tuweze kuwa watumishi wa agano jipya. Hili ni agano sio la barua bali ni la Roho. Kwa kuwa barua huua, lakini roho inatoa uhai.
7Sasa kazi ya kifo iliyokuwa imechongwa katika herufi juu ya mawe ilikuja kwa namna ya utukufu kwamba watu wa Israeli hawakuangalia moja kwa moja kwenye uso wa Musa. Hii ni kwa sababu ya utukufu wa uso wake, utukufu ambao ulikuwa unafifia.
8Je, kazi ya Roho haitakuwa na utukufu zaidi?
9Kwa kuwa kama huduma ya hukumu ilikuwa na utukufu, ni mara ngapi zaidi huduma ya haki huzidi sana katika utukufu!
10Ni kweli kwamba, kile kilichofanywa utukufu kwanza hakina utukufu tena katika heshima hii, kwa sababu ya utukufu unaouzidi.
11Kwa kuwa kama kile ambacho kilikuwa kinapita kilikuwa na utukufu, ni kwa kiasi gani zaidi kile ambacho ni cha kudumu kitakuwa na utukufu!
12Kwa kuwa tunajiamini hiyo, tunaujasiri sana.
13Hatuko kama Musa, aliyeweka utaji juu ya uso wake, ili kwamba watu wa Israel wasiweze kuangalia moja kwa moja kwenye mwisho wa utukufu ambao ulikuwa unatoweka.
14Lakini fahamu zao zilikuwa zimefungwa. Hata mpaka siku hii utaji uleule bado unabaki juu ya usomaji wa agano la kale. Haijawekwa wazi, kwa sababu ni katika Kristo pekee inaondolewa mbali.
15Lakini hata leo, wakati wowote Musa asomwapo, utaji hukaa juu ya mioyo yao.
16Lakini mtu anapogeuka kwa Bwana, utaji unaondolewa.
17Sasa Bwana ni Roho. Palipo na Roho wa Bwana, kuna uhuru.
18Sasa sisi sote, pamoja na nyuso zisizo wekewa utaji, huona utukufu wa Bwana. Tunabadilishwa ndani ya muonekano uleule wa utukufu kutoka shahada moja ya utukufu kwenda nyingine, kama ilivyo kutoka kwa Bwana, ambaye ni Roho.