Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 2 Wakorintho

2 Wakorintho 2

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Kwa hiyo niliamua kwa sehemu yangu mwenyewe kwamba nisingekuja tena kwenu katika hali ya uchungu.
2Kama niliwasababishia ninyi maumivu, ni nani angenifurahisha mimi, lakini ni yule ambaye aliumizwa na mimi?
3Niliandika kama nilivyofanya ili kwamba wakati nikija kwenu nisiweze kuumizwa na wale ambao wangekuwa wamenifanya nifurahi. Ninao ujasiri kuhusu ninyi nyote kwamba furaha yangu ni furaha ile ile mliyonayo ninyi nyote.
4Kwa kuwa niliwaandikia ninyi kutokana na mateso makubwa, na dhiki ya moyo, na kwa machozi mengi. Sikutaka kuwasababishia ninyi maumivu. Badala yake, nilitaka mjue upendo wa kina nilionao kwa ajili yenu.
5Kama kuna yeyote amesababisha maumivu, hajasababisha tu kwangu, lakini kwa kiwango fulani - bila kuweka ukali zaidi - kwenu ninyi nyote.
6Hii adhabu ya mtu huyo kwa wengi inatosha.
7Kwa hiyo sasa badala ya adhabu, mnapaswa kumsamehe na kumfariji. Fanyeni hivi ili kwamba asiweze kushindwa na huzuni iliyozidi.
8Kwa hiyo ninawatia moyo kuthibitisha upendo wenu hadharani kwa ajili yake.
9Hii ndiyo sababu niliandika, ili kwamba niweze kuwajaribu na kujua kuwa kama ni watii katika kila kitu.
10Kama mkimsamehe yeyote, na mimi pia namsamehe mtu huyo. Kile nilicho kisamehe - kama nimesamehe chochote-kimesamehewa kwa faida yenu katika uwepo wa Kristo.
11Hii ni kwamba Shetani asije akatufanyia madanganyo. Kwa kuwa sisi sio wajinga kwa mipango yake.
12Mlango ulifunguliwa kwangu na Bwana nilipokuja kwenye mji wa Troa kuhubiri injili ya Kristo pale.
13Hata hivyo, sikuwa na amani ya moyo, kwa sababu sikumkuta ndugu yangu Tito pale. Hivyo niliwaacha na nikarudi Makedonia.
14Lakini ashukuriwe Mungu, ambaye katika Kristo mara zote hutuongoza sisi katika ushindi. Kupitia sisi husambaza harufu nzuri ya maarifa yake mahala pote.
15Kwa kuwa sisi kwa Mungu, ni harufu nzuri ya Kristo, wote kati ya wale waliookolewa na kati ya wale wanaoangamia.
16Kwa watu ambao wanaangamia, ni harufu kutoka kifo hadi kifo. Kwa wale wanaookolewa, ni harufu nzuri kutoka uzima hadi uzima. Ni nani anayestahili vitu hivi?
17Kwa kuwa sisi sio kama watu wengi wanaouza neno la Mungu kwa faida. Badala yake, kwa usafi wa nia, tunanena katika Kristo, kama vile tunavyotumwa kutoka kwa Mungu, mbele ya Mungu.