Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 2 Wakorintho

2 Wakorintho 7

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Wapendwa wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizi, na tujitakase wenyewe kwa kila jambo ambalo linatufanya kuwa wachafu katika miili yetu na katika roho. Na tuutafute utakatifu katika hofu ya Mungu.
2Fanyeni nafasi kwa ajili yetu! Hatujamkosea mtu yeyote. Hatukumdhuru mtu yeyote. Hatujajinufaisha kwa faida ya mtu yeyote.
3Nasema hili siyo kwa kuwalaumu. Kwa kuwa nimeshasema kwamba mmo mioyoni mwetu, kwetu sisi kufa pamoja na kuishi pamoja.
4Nina ujasiri mwingi ndani yenu, na ninajivuna kwa ajili yenu. Nimejawa na faraja. Ninajawa na furaha hata katikati ya mateso yetu yote.
5Tulikuja Makedonia, miili yetu haikuwa na pumziko. Badala yake, tulipata taabu kwa namna zote kwa kupigwa vita upande wa nje na hofu upande wa ndani.
6Lakini Mungu, anayefariji waliokata tamaa, alitufariji kwa ujio wa Tito.
7Haikuwa kwa ujio wake tu kwamba Mungu alitufariji. ilikuwa pia faraja zile Tito alizopokea kutoka kwenu. Yeye alituambia upendo mkuu mlionao, huzuni yenu, na mlivyokuwa na wasiwasi kwa ajili yangu. Hivyo nimezidi kuwa na furaha zaidi.
8Hata ingawa waraka wangu uliwafanya kusikitika, mimi siujutii. lakini ninaujutia wakati nilipoona waraka huo uliwafanya ninyi kuwa na huzuni. lakini mlikuwa na huzuni kwa muda mfupi.
9Sasa nina furaha, si kwa sababu mlikuwa na shida, lakini kwa sababu huzuni zenu iliwaleta kwenye toba. Mlipatwa na huzuni ya kiungu, hivyo mliteswa si kwa hasara kwa sababu yetu.
10Kwa kuwa huzuni ya kiungu huleta toba ambayo hukamilisha wokovu bila ya kuwa na majuto. Huzuni ya kidunia, hata hivyo, huleta mauti.
11Angalieni huzuni hii ya kiungu ilizalisha azma gani kubwa ndani yenu. Jinsi gani azma ilikuwa kubwa ndani yenu kuthibitisha kuwa hamkuwa na hatia. Kwa jinsi gani uchungu wenu ulivyokuwa mkubwa, hofu yenu, matamanio yenu, bidii yenu, na shauku yenu kuona kwamba haki inapaswa kutendeka! Katika kila jambo mmethibitisha wenyewe kutokuwa na hatia.
12Ingawa niliwaandikia ninyi, sikuandika kwa ajili ya mkosaji, wala si kwa mtu aliyeteswa na maovu. Nimeandika ili kwamba udhati wa mioyo yenu kwa ajili yetu ifanywe kujulikana kwenu mbele ya macho ya Mungu.
13Ni kwa ajili ya hii kwamba tunafarijika. Katika nyongeza ya faraja yetu wenyewe, tunafurahi pia, hata zaidi kwa sababu ya furaha ya Tito, kwa kuwa roho yake iliburudishwa na ninyi nyote.
14Kwa kuwa kama nilijivuna kwake kuhusiana na ninyi, sikuwa na aibu. Kinyume chake, kama tu kila neno tulilolisema kwenu lilikuwa kweli, Majivuno yetu kuhusu ninyi kwa Tito yalithibitisha kuwa kweli.
15Upendo wake kwa ajili yenu hata ni mkubwa zaidi, kama akumbukapo utii wenu nyote, jinsi mlivyomkaribisha yeye kwa hofu na kutetemeka.
16Ninafurahi kwa sababu nina ujasiri kamili ndani yenu.