Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 2 Wakorintho

2 Wakorintho 6

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Na kwa hiyo, kufanya kazi pamoja, tunawasihi ninyi msiipokee neema ya Mungu pasipo matokeo.
2Kwa kuwa anasema, “Wakati uliokubalika nilikuwa makini kwenu, na katika siku ya wokovu niliwasaidia.” Tazama, sasa ni wakati uliokubalika. Tazama, sasa ni siku ya wokovu.
3Hatuweki jiwe la kizuizi mbele ya mtu yeyote, kwa kuwa hatuitakii huduma yetu iletwe katika sifa mbaya.
4Badala yake, tunajihakiki wenyewe kwa matendo yetu yote, kwamba tu watumishi wa Mungu. Tu watumishi wake katika wingi wa ustahimilivu, mateso, dhiki, ugumu wa maisha,
5kupigwa, vifungo, ghasia, katika kufanya kazi kwa bidii, katika kukosa usingizi usiku, katika njaa,
6katika usafi, maarifa, uvumilivu, wema, katika Roho Mtakatifu, katika upendo halisi.
7Tu watumishi wake katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu. Tuna silaha ya haki kwa ajili ya mkono wa kuuume na wa kushoto.
8Tunafanya kazi katika heshima na kudharauliwa, katika kashfa na sifa. Tunatuhumiwa kuwa wadanganyifu na wakati tu wakweli.
9Tunafanya kazi kana kwamba hatujulikani na bado tunajulikana vizuri. Tunafanya kazi kama wanaokufa na -Tazama! - bado tunaishi. Tunafanya kazi kama tunaoadhibiwa kwa ajili ya matendo yetu lakini sio kama waliohukumiwa hata kufa.
10Tunafanya kazi kama wenye masikitiko, lakini siku zote tuna furaha. Tunafanya kazi kama maskini, lakini tunatajirisha wengi. Tunafanya kazi kana kwamba hatupati kitu bali kama tunaomiliki kila kitu.
11Tumezungumza ukweli wote kwenu, Wakorintho, na mioyo yetu imefunguka kwa upana.
12mioyo yenu haizuiliwi na sisi, bali mnazuiliwa na hisia zenu wenyewe.
13Sasa katika kubadilishana kwa haki - ninaongea kama kwa watoto - fungueni mioyo yenu kwa upana.
14Msifungamanishwe pamoja na wasioamini. Kwa kuwa kuna uhusiano gani kati ya haki na uasi? Na kuna ushirika gani kati ya nuru na giza?
15Ni makubaliano gani Kristo anaweza kuwa nayo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na asiyeamini?
16Na kuna makubaliano gani yapo kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa kuwa sisi ni hekalu la Mungu aliye hai, kama ambavyo Mungu alisema: “Nitakaa kati yao na kutembea kati yao. Nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.”
17Kwa hiyo, “Tokeni kati yao, na mkatengwe nao,” asema Bwana. “Msiguse kitu kichafu, na nitawakaribisha ninyi.
18Nitakuwa Baba kwenu, nanyi mtakuwa wanangu wa kiume na wa kike,” asema Bwana Mwenyezi.