Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 2 Wakorintho

2 Wakorintho 8

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Tunawataka ninyi mjue, kaka na dada, kuhusu neema ya Mungu ambayo imetolewa kwa makanisa ya Makedonia.
2Wakati wa jaribu kubwa la mateso, wingi wa furaha yao na ongezeko la umaskini wao umezaa utjiri mkubwa wa ukarimu.
3Kwa maana nashuhudia kwamba walitoa kwa kadiri ya walivyoweza, na hata zaidi ya walivyoweza.
4Na kwa hiari yao wenyewe kwa kutusihi kwingi, walituomba kwa ajili ya kushiriki katika huduma hii kwa waumini.
5Hii haikutokea kama tulivyokuwa tunatarajia. Badala yake, kwanza walijitoa wao wenyewe kwa Bwana. Kisha wakajitoa wao wenyewe kwetu kwa mapenzi ya Mungu.
6Hivyo tulimsihi Tito, aliyekuwa tayari ameanzisha kazi hii, kuleta katika utimilifu tendo hili la ukarimu juu yenu.
7Lakini ninyi mna wingi katika kila kitu- katika imani, katika usemi, katika maarifa, katika bidii, na katika upendo wenu kwa ajili yetu. Hivyo hakikisheni kwamba ninyi mnakuwa na wingi pia katika tendo hili la ukarimu.
8Nasema hili si kama amri. Badala yake, nasema hili ili kupima uhalisi wa upendo wenu kwa kuulinganisha na shauku ya watu wengine.
9Kwa maana mnajua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo. Hata kama alikuwa tajiri, kwa ajili yenu alikuwa maskini. Ili kwamba kupitia umaskini wake mweze kuwa tajiri.
10Katika jambo hili nitawapa ushauri ambao utawasaidia. Mwaka mmoja uliopita, hamkuanza tuu kufanya jambo. Lakini mlitamani kulifanya.
11Sasa likamilisheni. Kama tu kulivyokuwa na shauku na nia ya kulifanya, kisha, je, mngeweza pia kulileta katika ukamilifu, kwa kadri ya mnavyoweza.
12Kwa kuwa mnashauku ya kufanya tendo hili, ni jambo zuri na linakubalika. Lazima lisimame juu ya kile alichonacho mtu, siyo juu ya asichokuwa nacho mtu.
13Kwa kuwa kazi hii siyo kwa ajili kwamba wengine waweze kupata nafuu na ninyi mweze kulemewa. Badala yake, kuwe na usawa.
14Wingi wenu wa wakati wa sasa utasaidia kwa kile wanachohitaji. Hii ni hivyo pia ili kwamba wingi wao uweze kusaidia mahitaji yenu, na kwamba kuwe na usawa.
15Hii ni kama ilivyoandikwa; “Yeye aliye na vingi hakuwa na kitu chochote kilichobaki na yeye aliyekuwa na kidogo hakuwa na uhitaji wowote.”
16Lakini ashukuriwe Mungu, aliyeweka ndani ya moyo wa Tito moyo uleule wa bidii ya kujali ambyo ninayo kwa ajili yenu.
17Kwa kuwa si tu alipokea maombi yetu, bali pia alikuwa na bidii kuhusiana na maombi hayo. Alikuja kwenu kwa hiari yake mwenyewe.
18Tumemtuma pamoja naye ndugu ambaye anasifiwa miongoni mwa makanisa kwa ajili ya kazi yake katika kutangaza injili.

19Si hivi tu, lakini pia alichaguliwa na makanisa kusafiri nasisi katika kulibeba sehemu mbalimbali tendo hili la ukarimu. Hii ni kwa utukufu wa Bwana mwenyewe na kwa shauku yetu ya kusaidia.
20Tunaepuka uwezekano kwamba yeyote napaswa kulalamika kuhusiana na sisi kuhusiana na ukarimu huu ambao tunaubeba.
21Tunachukua uangalifu kufanya kilicho cha heshima, sio tu mbele za Bwana, lakini pia mbele za watu.
22Pia tunamtuma ndugu mwingine pamoja nao. Tumempima mara nyingi, na tumemwona ni mwenye shauku for ajili ya kazi nyingi. Hata sasa ana bidii zaidi kwa sababu ya ujasiri mkubwa alionao ndani yenu.
23Kwa habari ya Tito, yeye ni mshirika mwenza wangu na mtendakazi mwenzangu kwa ajili yenu. Kama kwa ndugu zetu, wanatumwa na makanisa. Ni waheshima kwa Kristo.
24Hivyo, waonesheni upendo wenu, na muoneshe kwa makanisa sababu ya majivuno yetu kwa ajili yenu.