Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Malaki

Malaki 3

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Tazama, namtuma mjumbe wangu, atakayeandaa njia mbele yangu. Na Bwana, ambaye mnamtafuta, atakuja ghafla katika hekalu lake; na mjumbe wa agano, ambaye katika yeye mnafurahi, tazama anakuja.” asema Bwana wa Majeshi.
2Na ni nani atakeyevumilia siku ya kuja kwake? na nani atasimama akishatokea? Yeye ni kama mtu asafishaye kwa moto na kama sabuni ya kufulia.
3Atakaa na kutawala kama msafishaji wa fedha, na atawasafisha wana wa Lawi. na atawafanya wawe safi kama dhahabu na fedha, na wataleta sadaka za haki kwa Bwana.
4Na sadaka ya Yuda na Yerusalem itampendeza Bwana, kama siku za kale, na miaka ya zamani.
5Kisha nitapita karibu na ninyi kuwahukumu. na nitakuwa shahidi mwepesi dhidi ya wachawi, wazinzi, mahsahidi wa uongo, na kinyume cha wale wanaoonea wafanyakazi katika mizigo yake, wanaoonea wajane na yatima, na anayemfukuza mgeni kutoka kwenye haki yake, na kwa wale wasionitii mimi,” asema Bwana wa majeshi.
6Mimi Bwana, sibadiliki; pia ninyi, watu wa Yakobo, hamkutumia.
7Toka siku za baba zenu mmegeukia mbali na amri zangu na hamkuzitunza. Nigeukieni, nami nitawarudia ninyi,” asema Bwana wa majeshi. Lakini mwasema, tutakurudiaje?
8Mwanadamu anaweza kumwibia Mungu? Mnaniibia mimi, lakini mwasema, 'Tumekuibiaje?' kwa zaka na sadaka.
9Mmelaani kwa laana, kwa kuniibia mimi, taifa lote hili.
10Leteni zaka kamili katika ghalani, ili kwamba kiwemo chakula katika nyumba yangu. Na mnijaribu kwa hili,” asema Bwana wa Majeshi. “kama sitawafungulia madilisha ya mbinguni na kuwamwagia baraka juu yenu, ili kwamba hakutakuwa na sehemu ya kutosha kuzipokea.
11Nitamkemea mharibifu kwako, kwamba asiharibu mavuno yenu ya nchi yenu; mizazibu yenu katika shamba haitapukutisha kabla ya wakati wake,” asema Bwana wa Majeshi.
12Mataifa yote watakuita mbarikiwa; kwa ajili yako itakuwa ni nchi ya furaha,” asema Bwana wa Majeshi.
13Maneo yenu yamekuwa magumu kinyume changu,” asema Bwana. lakini mwasema, “Tumesema nini kinyume chako?'
14mmesema, 'Hakuna maana kumtumikia Mungu. Kuna faida ya namna gani kutunza maagizo yake au kutembea huku mkiomboleza mbele za Bwana wa Majeshi?
15Na sasa tunamwita mwenye kiburi mbarikiwa. Waharifu si kufanikiwa tu, bali kumjaribu Mungu na kumwepuka.”
16Kisha wale wanaomweshimu Bwana walisemezana mmoja baada ya mwingine; Bwana yuko makini kutusikiliza, na kitabu cha kumbukumbu kiliandikwa mbele zake kwa ajili ya wale wanamwogopa Bwana na kuliheshimu jina lake.
17“Watakuwa wangu,” asema Bwana wa majeshi,” hazina zangu, katika siku nitakayotenda; nitawapenda, kama mtu anavyompenda mwanawe anayemhudumia.
18Kisha zaidi sana nitatofautisha kati ya haki wenye haki na waovu, kati ya anayemwabudu Mungu na asiyemwabudu yeye.