Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Malaki

Malaki 4

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Tazama, siku inakuja, inaka kama tanuru, ambayo wote wenye kiburi na waharifu watakuwa mabua. siku inakuja itawachoma,” asema Bwana wa Majeshi, “siku hiyo itaondoa mzizi au shina.
2Lakini kwenu mnaoliogopa jina langu, jua la haki litawaangazia na uponyaji katika mbawa zake. Mtarukaruka kama ndama zizini.
3Na waovu wote mtawakanyaga chini, watakuwa majivu chini ya nyazo za miguu yenu siku hiyo nitatenda,” asema Bwana wa Majeshi.
4“Kumbukeni kutii sheria za mtumishi wangu Musa, mmri na sheria nilizomwamuru huko Horebu, kwa Israel wote.
5Tazama, nitamtuma Eliya nabii mbele ya siku kuu na yenye kutisha ya kuja kwa Bwana.
6Atarudisha moyo wa baba kwa watoto, na mioyo ya watoto kwa baba zao; ili kwamba nisije nikaiangamiza nchi kwa uharibifu wote.”