Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Luka - Luka 2

Luka 2:20-46

Help us?
Click on verse(s) to share them!
20Wachungaji wakarudi wakimtukuza na kumsifu Mungu kwa ajili ya kila kitu walichokwisha sikia na kuona, kama tu ilivyokuwa imenenwa kwao.
21Ilipofika siku ya nane na ilikuwa ni wakati wa kumtahiri mtoto, wakamwita jina Yesu, jina alilokwishapewa na yule malaika kabla mimba haijatungwa tumboni.
22zao zilizotakiwa za utakaso zilipopita, kulingana na sheria ya Musa, Yusufu na Mariamu wakampeleka hekaluni kule Yerusalemu kumweka mbele za Bwana.
23Kama ilivyoandikwa katika sheria ya Bwana, “Kila mwanaume anayefungua tumbo ataitwa aliyetolewa wakfu kwa Bwana.”
24Wao vilevile walikuja kutoa sadaka kulingana na kile kinachosemwa katika sheria ya Bwana, “Jozi ya njiwa au makinda mawili ya njiwa.”
25Tazama, palikuwa na mtu katika Yerusalemu ambaye jina lake alikuwa akiitwa Simeoni. mtu huyu alikuwa mwenye haki na mcha Mungu. Yeye alikuwa akisubiri kwa ajili ya mfariji wa Israeli, na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake.
26Ilikuwa imekwisha funuliwa kwake kupitia Roho Mtakatifu kwamba yeye hangelikufa kabla ya kuwomwona Kristo wa Bwana.
27Siku moja alikuja ndani ya hekalu, akiongozwa na Roho Mtakatifu. Ambapo wazazi walimleta mtoto, Yesu, kumfanyia yale yaliyopasa kawaida ya sheria,
28ndipo Simeoni alimpokea mikononi mwake, na akamsifu Mungu na kusema,
29“Sasa ruhusu mtumishi wako aende kwa amani Bwana, kulingana na Neno lako.
30Kwa kuwa macho yangu yameuona wakovu wako,
31ambao umeonekana kwa macho ya watu wote.
32Yeye ni nuru kwa ajili ya ufunuo kwa Wamataifa na utukufu wa watu Israeli.”
33Baba na Mama wa mtoto walishangazwa kwa mambo ambayo yalizungumzwa juu yake.
34Ndipo Simeoni akawabariki na akasema kwa Mariamu mama yake, “Sikiliza kwa makini! Mtoto huyu atakuwa sababu ya kupotea na kuokoka kwa watu wengi katika Israeli na ni ishara ambayo watu wengi wataipinga.
35Pia ni upanga utakaochoma nafsi yako mwenyewe, ili kwamba mawazo ya mioyo ya wengi yadhihirike”.
36Nabii mwanamke aliyeitwa Ana pia alikuwako hekaluni. Yeye alikuwa binti wa Fanueli kutoka kabila la Asheri. Alikuwa na miaka mingi sana. Naye aliishi na mume wake kwa miaka saba baada ya kuoana,
37na ndipo akawa mjane kwa miaka themanini na minne. Naye hakuwahi kuondoka hekaluni na alikuwa akiendelea kumwabudu Mungu pamoja na kufunga na kuomba, usiku na mchana.
38Na kwa wakati huo, alikuja pale walipo akaanza kumshukuru Mungu. Aliongea kumhusu mtoto kwa kila mtu ambaye alikuwa akisubiri ukombozi wa Yerusalemu.
39Walipomaliza kila kitu walichotakiwa kufanya kuligana na na sheria ya Bwana, walirudi Galilaya, mjini kwao, Nazareti.
40Mtoto alikua, na akawa na nguvu, akiongezeka katika hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake.
41Wazazi wake kila mwaka walikwenda Yerusalemu kwaajili ya sikukuu ya Pasaka.
42Alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, walikwenda tena wakati mwafaka kidesturi kwa ajili ya sikukuu.
43Baada ya kubaki siku zote kwa ajili ya sikukuu, walianza kurudi nyumbani. Lakini mvulana Yesu alibaki nyuma mle Yerusalemu na wazazi wake hawakujua hili.
44Walidhani kwamba yumo kwenye kundi walilokuwa wakisafiri nalo, hivyo walisafiri safari ya siku. Ndipo wakaanza kumtafuta miongoni wa ndugu na marafiki zao.
45Waliposhindwa kumpata, walirudi Yerusalemu na wakaanza kumtafuta humo.
46Ikatokea kwamba baada ya siku tatu, wakampata hekaluni, akiwa ameketi katikati ya waalimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali.

Read Luka 2Luka 2
Compare Luka 2:20-46Luka 2:20-46