Text copied!
CopyCompare
Biblia Takatifu - Luka - Luka 20

Luka 20:30-45

Help us?
Click on verse(s) to share them!
30Yule ndugu wa pili akamwoa yule mjane, naye pia, akafa;
31na ndugu wa tatu vilevile. Mambo yakawa yaleyale kwa wote saba—wote walikufa bila kuacha watoto.
32Mwishowe akafa pia yule mwanamke.
33Je, siku wafu watakapofufuliwa, mwanamke huyo atakuwa mke wa nani? Alikuwa ameolewa na wote saba.”
34Yesu akawaambia, “Watu wa nyakati hizi huoa na kuolewa;
35lakini wale ambao Mungu atawawezesha kushiriki ule wakati wa ufufuo, hawataoa wala kuolewa.
36Ama hakika, hawawezi kufa tena, kwa sababu watakuwa kama malaika, na ni watoto wa Mungu kwa vile wamefufuliwa katika wafu.
37Lakini, kwamba kuna kufufuka kutoka wafu, hata Mose alithibitisha jambo hilo katika Maandiko Matakatifu. Katika sehemu ya Maandiko Matakatifu juu ya kile kichaka kilichokuwa kinawaka moto, anamtaja Bwana kama Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo.
38Basi, yeye si Mungu wa wafu, bali ni Mungu wa wale walio hai; maana wale aliowaita kwake, wanaishi naye.”
39Baadhi ya wale walimu wa Sheria wakasema, “Mwalimu, umejibu vema kabisa.”
40Walisema hivyo kwa sababu hawakuthubutu kumwuliza tena maswali mengine.
41Yesu akawauliza, “Yasemekanaje kwamba Kristo ni mwana wa Daudi?
42Maana Daudi mwenyewe anasema katika Zaburi: Bwana alimwambia Bwana wangu: Keti upande wangu wa kulia
43mpaka niwafanye adui zako kama kiti cha kuwekea miguu yako.
44Ikiwa Daudi anamwita yeye, Bwana, basi atakuwaje mwanawe?”
45Yesu aliwaambia wanafunzi wake mbele ya watu wote,

Read Luka 20Luka 20
Compare Luka 20:30-45Luka 20:30-45