Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Luka - Luka 20

Luka 20:19-34

Help us?
Click on verse(s) to share them!
19Hivyo waandishi na wakuu wa makuhani walitafuta njia ya kumkamata wakati huohuo, walijua kwamba alikuwa amesema mfano huu dhidi yao. Lakini waliwaogopa watu.
20Walimuangalia kwa makini, wakatuma wapelelezi waliojifanya kuwa watu wa haki, ili wapate kupata kosa kwa hotuba yake, ili kumpelekakwa watawala na wenye mamlaka.
21Nao wakamwuliza, wakisema, “Mwalimu, tunajua kwamba unasema na kufundisha mambo ya kweli na si kushawishiwa na mtu yeyote, lakini wewe hufundisha ukweli kuhusu njia ya Mungu.
22Je, ni halali kwetu kulipa kodi kwa Kaisari, au la?”
23Lakini Yesu alitambua mtego wao, akawaambia,
24“Nionyesheni dinari. Sura na chapa ya nani ipo juu yake?” Walisema, '“Ya Kaisari.”
25Naye akawaambia, 'Basi, mpeni Kaisari yaliyo yake Kaisari, na Mungu yaliyo yake Mungu.'
26Waandishi na wakuu wa makuhani hawakuwa na uwezo wa kukosoa kile alichosema mbele ya watu. Wakastaajabia majibu yake na hawakusema chochote.
27Baadhi ya Masadukayo wakamwendea, wale ambao wanasema kwamba hakuna ufufuo,
28wakamwuliza, wakisema, “Mwalimu, Musa alituandikia kwamba kama mtu akifiwa na ndugu mwenye mke ambaye hana mtoto basi anapaswa kumchukuna mke wa ndugu yake na kuzaa nae kwa ajili ya kaka yake.
29Kulikuwa na ndugu saba Wa kwanza alioa, akafa bila kuacha mtoto,
30na wa pili pia.
31Wa tatu akamchukua vilevile, vivyo hivyo wa saba hakuacha watoto na akafa.
32Baadaye yule mwanamke pia akafa.
33Katika ufufuo atakuwa mke wa nani? Maana wote saba walikuwa wamemwoa.'
34Yesu akawaambia, “Wana wa ulimwengu huu huoa na kuolewa.

Read Luka 20Luka 20
Compare Luka 20:19-34Luka 20:19-34