66Na wote walioyasikia wakayatunza mioyoni mwao, wakisema, “Mtoto huyu kuwa wa namna gani?” Kwasababu mkono wa Bwana ulikuwa pamoja naye.
67Baba yake Zekaria alijazwa na Roho Mtakatifu na akatoa unabii, akisema,
68“Asifiwe Bwana, Mungu wa Israeli, kwa sababu amesaidia na alishughulikia wokovu kwa watu wake.
69Ametuinulia pembe ya wokovu katika nyumba ya mtumishi wake Daudi, kutoka miongoi mwa mwa ukoo wa mtumishi wake Daudi,
70kama alivyosema kwa kinywa cha manabii wake waliokuweko katika nyakati za kale.
71Atatuoka kutoka kwa adui zetu na kutoka mikononi mwa wote wanaotuchukia.
72Atafanya hivi kuonesha rehema kwa baba zetu, na kukumbuka agano lake takatifu,
73kiapo alichokisema kwa Abrahamu baba yetu.
74Aliapa kuthibitha kwamba ingewezekana kumtumikia Yeye bila hofu, baada ya kuokolewa kutoka katika mikononi ya adui zetu.
75katika utakatifu na haki mbele zake siku zetu zote.
76Ndiyo, na wewe mtoto, utaitwa nabii wa Aliye Juu Sana, kwa kuwa utaenenda mbele za uso wa Bwana ili kumwandalia njia, kuwaandaa watu kwa ajili ya ujio wake,
77kuwafahamisha watu wake kwamba, wataokolewa kwa njia ya kusamehewa dhambi zao.