51Kila hema litakapotakiwa kuhamishiwa eneo jingine, Walawi ndio watakaolipeleka pale. Na kila hema litakapotakiwa kusimamishwa, Walawi ndio watakao lisimamisha. Na mgeni yeyote atakayelisogelea hema lazima auawe.
52Wakati watu wa Israeli watakaposimamisha hema zao, kila mwanaume lazima awe karibu na bango la jeshi lake.
53Hata hivyo Walawi lazima waweke hema zao kuizunguka hiyo masikani ya amri za agano ili kwamba hasira yangu isije ikawaka juu ya wana wa Israeli. Walawi lazima wailinde hiyo masikani ya amri za agano.”