Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Hesabu - Hesabu 1

Hesabu 1:4-16

Help us?
Click on verse(s) to share them!
4Kila mwanamume kwa kila kabila, kichwa cha ukoo, lazima atumike na wewe kama kiongozi wa kabila.
5Haya ndiyo majina ya viongozi ambao watapigana pamoja na wewe: Kutoka kabila la Reubeni, Elizuri mwana wa Shedeuri;
6kutoka kabila la Simeoni, Shelumiel mwana wa Zurishadai
7Kutoka kabila la Yuda, Nashoni mwana wa Aminadabu;
8Ktoka kabila la Isakari, Nethaneli mwana wa Zuari;
9kutoka kabila Zebuluni, Eliabu mwana wa Heloni
10kutoka kabila la Efraimu mwana wa Yusufu, Elishama mwana wa Ammihudi; kutoka kabila la Manase, Gamaliel mwan wa Pedazuri;
11kutoka kabila la Benjamini mwana wa Ysufu, Abidani mwan wa Gidion;
12Kutoka kabila la Dan, Ahizeri mwana wa Amishadai;
13kutoka kabila Asheri, Pagieli mwana wa Okirani;
14kutoka kabila la Gadi, Eliasafu mwana wa Deuli;
15na kutoka kabila la Naftali, Ahira mwana wa Enani.”
16Hawa ndio wanaume waliochaguliwa kutoka kwa watu. Waliongoza kabila za mababu zao. Walikuwa viongozi wa koo katika Israel.

Read Hesabu 1Hesabu 1
Compare Hesabu 1:4-16Hesabu 1:4-16