Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zekaria

Zekaria 11

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Fungua milango yako, ee Lebanoni, ili moto uteketeze mielezi yako!
2Omboleza, enyi miti ya misonobari, kwani mierezi imeanguka! Kilichokuwa cha fahari kimeteketezwa! Ombolezeni, enyi mialoni ya Bashani, kwani msitu wenye nguvu umeshushwa.
3Wachungaji wanapiga yowe, kwa kuwa utukufu wao umeharibiwa! Sauti ya mungurumo wa wana simba, kwa kuwa kiburi cha Mto Yordani kimeharibiwa!
4Hivi ndivyo asemavyo Yahwe Mungu wangu, “Lichungeni kundi la kondoo lililotiyari kuchinjwa!
5(Wanaowanunua wanawachinja bila kuhadhibiwa, nao wawauzao husema, 'Atukuzwe Yahwe! Nimetajirika! Kwa maana wachungaji wafanyao kazi kwa wenye kondoo hawawahurumii.)
6Kwa maana hiyo sitawahurumia tena wenyeji wa nchi! - hivi ndivyo asemavyo Yahwe. Tazama! Mimi mwenyewe nipo tiyari kumwelekeza kila mtu katika mkono wa jirani yake na katika mkono wa mfalme wake, nao wataiharibu nchi na hakuna hata mmoja wao nitakayemwokoa kutoka katika mkono wao.”
7Hivyo nikawa mchungaji wa kondoo walioamriwa kuchinjwa, kwa wanaowashughulikia kondoo. Nilichukua fimbo mbili; fimbo moja nikaiita “Neema” na nyingine nikaiita “Umoja.” Kwa njia hii niliwachunga kondoo.
8Ndani ya mwezi mmoja niliwaangamiza wachungaji watatu, kwa maana sikuwavumilia tena, wao pia walinichukia.
9Ndipo nilipowaambia wamiliki, “Sitafanya kazi kama mchungaji wenu tena. Wakondoo wafao - na wafe; kondoo wanaoangamizwa - na waangamizwe. Na kondoo wasaliao kila mmoja ale nyama ya jirani yake.”
10Hivyo nikaichukua fimbo yangu “Neema” na nikaivunja kuvunja agano nililokuwa nimelifanya na kabila zangu zote.
11Katika siku hiyo agano lilivunjwa, na wale wanaoshughulika na kondoo na waliokuwa wakiniangalia walifahamu kwamba Yahwe amesema.
12Nikawaambia, “Ikiwa itawapendeza, nilipeni ujira wangu. Kama sivyo, msifanye hivyo.” Hivyo wakapima ujira wangu - vipande thelathini vya fedha.
13Kisha Yahwe akaniambia, “Weka fedha katika hazina, thamani nzuri zaidi ambayo walikupa!” Hivyo nikachukua vipande thelathini vya fedha na kuviweka katika hazina ndani ya nyumbani Yahwe.
14Kisha nikavunja fimbo yangu ya pili, “Umoja,” kuvunja undugu kati ya Yuda na Israeli.
15Yahwe akaniambia, “Tena, chukua chombo cha mchungaji mpumbavu kwa ajili yako mwenyewe,
16kwa maana tazama, niko tiyari kumweka mahali mchungaji katika nchi. Hataangalia kondoo wanaoangamia. Hatatafuta kondoo wapoteao, wala kuwaponya kondoo wachechemeao. Hatawalisha kondoo wenye afya, lakini atakula nyama ya kondoo walionona naye atapasua kwato zao.
17Ole kwa wachungaji wasiofaa wanaoliacha kundi la kondoo! Upanga na uje dhidi ya mkono wake na jicho lake la kulia! Mkono wake na ukauke na jicho lake la kulia lipofuke!